Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue azindua timu ya wataalam wa serikali wa kufanya mazungumzo katika mikataba ya gesi asilia na mafuta
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza wakati wa kuzindua timu
ya wataalam wa mazungumzo katika mikataba ya gesi na mafuta kutoka
serikalini na mafunzo yao maalum yaliyofanyika katika hoteli ya Park
Hyatt kisiwani Zanzibar jana. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk. Abdulhamid Yahya Mzee na Bi.
Sheila Khama Mkurugenzi wa Kituo cha Rasilimali za Afrika katika Benki
ya Maendeleo ya Afrika.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa UONGOZI Institute Profesa Joseph Semboja akitoa hotuba
ya kumkaribisha mgeni rasmi na wageni waalikwa katika uzinduzi wa timu
hiyo ya wataalam wa mazungumzo katika mikataba ya gesi na mafuta ambao
umeenda sambamba na mafunzo maalum ya siku mbili kisiwani Zanzibar.
UONGOZI Institute ikishirikiana na Chuo Kikuu cha Columbia (Taasisi ya Uwekezaji Endelevu) na Mradi wa Wanasheria Waandamizi wa Kimataifa ndio
waandaji wakuu wa timu hiyo ya wataalam ambao watapitia mafunzo ya
miezi sita katika masuala ya yatakayowanoa kupata mikataba bora ya
mafuta na gesi asilia kwa manufaa bora ya nchi.
Taswira ya wageni waalikwa pamoja na washiriki wa mafunzo ya wataalam wa mazungumzo katika mikataba ya gesi na mafuta. Wataalam ishirini
na tano waliochaguliwa kuingia katika timu ya mazungumzo wanatoka
katika ofisi na taasisi mbali mbali kama Wizara ya Nishati na Madini,
Wizara ya Fedha, Wizara ya Kazi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,
TANESCO, TPDC, Tume ya Mipango, STAMICO, Ofisi ya Waziri Mkuu, Benki
Kuu, TRA, Wizara ya Viwanda na Biashara, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
TAMISEMI na NEMC.
Mjadala wa mafuta na gesi ukiendelea.
No comments:
Post a Comment