JIJI LA DAR LAJAA MAJI
Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii.
MAFURIKO,Mafuriko,Mafuriko .! Jiji la Dar limejaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha wengine kukosa makazi.
Maeneo
yaliyokumbwa kwa mafuriko ni Mnyamani (Ilala),Bonde la Mpunga
(Kinondoni) ,Kigogo (Kinondoni),Mikocheni ( Kinondoni),Vingunguti
(Ilala) Tabata Kisiwani (Ilala)na Kurasini (Temeke) na maeneo mengine
ambayo hayajawahi kupata mafuriko yamefika.
Mvua
hizo zimeharibu miundombinu katika barabara ya Morogoro kwa kujaa maji
na kufanya kutokuwepo kwa usafiri kuelekea katikati ya jiji la Dar es
Salaam.
Kwa
Wilaya Ilala ni eneo moja ndilo limekuwa likisababisha mafuriko, ni kwa
wale waliojenga karibu na bonde la mto Msimbazi ndio wamekuwa
waathirika wa mafuriko kila mwaka.
Wananchi
wa maeneo yaliyokumbwa na mafuriko hawana msaada wowote huku mvua
ikiendelea kunyesha kuanzia majira ya saa 10 jioni na kuamkia leo hadi
katika muda huu mvua inatikisa.
Akizungumza
na Ripota wa Globu ya Jamii,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck
Sadick amesema kuwa serikali msaada wake ni wale waliopata madhara
kutokana na mvua hizo na sio kuwapa makazi na chakula kutokana na
kukataa kuhama maeneo hayo na kuishia kuipeleka serikali mahakamani.
Mkuu
wa Mkoa amesema serikali ilitoa maeneo mbadala ya kwenda kujenga na
kuishi kwa watu wa maeneo ambayo mara kwa mara wamekuwa wakipata
mafuriko, walikataa na kuipeleka serikali mahakamani hivyo sasa haiwezi
kuwasaidia.
“Sasa
sisi tufanye nini tutawaombea sala,lakini msaada kwetu ni wale
waliopata madhara ya kiafya kwa ajili matibabu,Serikali ndio itafanya
hivyo”amesema Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina
wa Jeshi la Polisi (CP),Suleiman Kova amesema katika mvua zinazoendelea
mtu mmoja amepoteza maisha kwa kuanguka katika mto ng’ombe uliyopo eneo
la Mburahati jijini Dar es Salaam.
Kamanda
Kova amesema aliyepoteza maisha ni Shaban Idd (73) Mkazi wa Manzese
jijini Dar es Salaam na mwili wake umeopolewa na kuhifadhiwa Hospitali
ya Mwananyamala.
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
No comments:
Post a Comment