ILO Tanzania yaadhimisha miaka 5 ya kuwawezesha vijana Tanzania kupitia ujasiriamali.
Naibu waziri wa kazi
na ajira, Mheshimiwa Makongoro Mahanga akimkabidhi cheti cha kutambua mchango
wa serikali ya Zanzibar katika mradi wa ujasiriamali, ndugu Ameir Ali Ameir,
ambaye ndiye Mkurugenzi wa Ajira kutoka Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma,
Zanzibar.
Mkurugenzi wa Ajira
kutoka Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma, Zanzibar.ndugu Ameir Ali Ameir
akizungumza na waandishi wa habari.
Mkurugenzi Mkuu wa
ILO Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda Bwana Alexio Musindo akizungumza na
waandishi wa habari.
Naibu waziri wa kazi
na ajira, Mheshimiwa Makongoro Mahanga akizungumza na waandishi wa habari.
Baadhi
ya wahudhuriaji wa kongamano la kuadhimisha Miaka mitano ya mradi wa
Ujasiriamali uliokuwa unaendeshwa na Shirika la Kazi la Kimataifa
(ILO).
Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Philippe Poinsot akizungumza wakati wa kongamano
Mshauri Mkuu wa Ufundi wa Mradi, Bwana Jealous Chirove, akielezea mafanikio ya mradi
ILO Tanzania yaadhimisha miaka 5 ya
kuwawezesha vijana Tanzania kupitia ujasiriamali. Shirika
la Kazi la Kimataifa (ILO) leo limeadhimisha miaka 5 toka kuanzishwa kwa mfuko
wa ujasiriamali wa vijana (YEF) kwa kuandaa kongamano katika ukumbi wa Mwalimu
Julius Nyerere.
Mfuko
wa Ujasiriamali kwa vijana ulizinduliwa mwaka 2010 ukilenga katika kutengeneza
ajira kwa vijana kwa kupitia ukuzaji wa sekta binafsi pamoja na kuongeza
ushindani kwenye uchumi wa Afrika.
Mradi
ulijikita katika kuwatengenezea vijana ajira nzuri, kukuza ujasiriamali na
kuwatengenezea fursa vijana wa kiafrika kupitia elimu, kuwaongezea ujuzi na
uwezeshaji wa mtaji. Kwa
kupitia mradi huu wa Kuwezesha Ujasiriamali, Mfuko wa Ujasiriamali kwa vijana
ulilenga kutengeneza maelfu ya ajira kwa vijana katika nchi za Kenya, Tanzania
na Uganda.
Msingi
mkuu wa mradi ulikuwa kukuza utamaduni wa ujasiriamali miongoni mwa vijana,
kuingiza elimu ya ujasiriamali katika mitaala, kuongeza uwingi wa mambo
yanayowezekana katika ajira kwa vijana, kuwezesha taasisi za vijana kutekeleza
mawazo mazuri ya ujasiriamali na kuwezesha upatikanaji wa mitaji kwa vijana
walio nje ya shule.
Toka
mradi umeanzishwa, umewezesha zaidi ya vijana 30,000 ambao ni wajasiamarali
wapya na waliopo kupitia utoaji wa elimu ya biashara, kusaidia uanzishwaji wa
biashara zaidi ya 17,000 pamoja na utengenezaji wa zaidi ya ajira 40,000 kwa
vijana, ambayo vyote kwa pamoja vimevuka malengo ya mradi yaliyoaninishwa
mwanzo.
No comments:
Post a Comment