WAMEONDOKA NA BONGO MUVI YAO!
Marehemu Steven Charles Kanumba enzi za uahi wake.
Kwenye familia yangu mama alipotangulia mbele ya haki, familia
ilikuwa juu mno kwa kila kitu lakini ghafla iliyumba vibaya hivyo
tukapata kazi ya kuisimamisha upya, jambo ambalo limekuwa gumu kufikia
pale tulipokuwa awali. Ishu hapa ni mchango wa mtu katika eneo lake.
Anapoondoka ni lazima ‘gepu’ lake huonekana na kuliziba inahitaji nguvu
kubwa na ya ziada.Kanumba
Aprili 7, mwaka huu ilikuwa ni siku ya kumbukumbu ya miaka mitatu tangu alipofariki dunia nguli wa sinema za Kibongo, marehemu Steven Charles Kanumba.
Ni katika kipindi ambacho mastaa wa tasnia hiyo wamekuwa wakiangua vilio kwamba sinema za nyumbani kwa sasa haziuzi. Kwa kifupi hazilipi!
Wapo waliokiri waziwazi kuwa kuondoka kwa staa huyo kumeliangusha soko hilo kwa kuwa ushindani aliouonesha na mwigizaji mwenzake, Vincent Kigosi ‘Ray’ haupo tena. Na wengine nao wamekosa ile chachu ya moyo wa ushindani. Matokeo yake wamebaki palepale siku zote na wengine kunyamaza kabisa. Hawasikiki!
Marehemu Adam Kuambiana enzi za uhai wake.
Ukweli ni kwamba mastaa wengi wa tasnia hiyo kwa sasa wanaishi maisha
magumu ya kuungaunga. Wana majina makubwa lakini hawana kodi za nyumba.
Wamebaki na magari yaleyale ambayo sasa yanawatoa jasho kujaza mafuta
na kuyafanyia matengenezo. Yamekuwa mikweche. Wamebaki kuombaomba.Mastaa mbalimbali wamekiri hili:
JB
Jacob Steven ‘JB’ ni mmoja wa waigizaji wakubwa Bongo ambao wanauza zaidi hasa anapokuwa na mchekeshaji Amri Athuman ‘Mzee Majuto’.Kwa mujibu wa JB tasnia ya filamu inaangukia katika kifo kutokana na kwamba kwa sasa haziuzi na uwepo wa maharamia.JB anasema kuwa hali hiyo inawafanya wasambazaji kuanza kuikimbia tasnia hiyo na wengine kushusha bei ya filamu.
Dude
Kauli ya JB inaungwa mkono na mwigizaji mwingine mkubwa, Kulwa Kikumba ‘Dude’ ambaye anaamini kuwa kuna kitu cha kufanya ikiwemo watu kuwekeza kwenye tasnia hiyo. Pia kuna suala la elimu kwa waigizaji, madairekta, maprodyuza na wasambazaji wazawa kisha serikali itenge bajeti kama ilivyo kwa Nollywood (Nigeria) na Hollywood (Marekani) kwa kuwa ni tasnia inayoajiri watu wengi.
Dk. Cheni
Mara kadhaa, mwigizaji Mausen Awadh ‘Dk. Cheni’ amekuwa akionesha wasiwasi wake juu ya kudorora kwa tasnia hiyo. Wapo baadhi ya waigizaji ambao hawakubali ukweli lakini Dk. Cheni ni miongoni mwa watu wa mwanzo kabisa waliokiri kwamba kifo cha Kanumba kiliathiri kwa kiasi kikubwa tasnia ya sinema Bongo.Mbali na Kanumba, pia wapo maprodyuza na madairekta waliotangulia mbele ya haki.
Adam Kuambiana
Ukizungumza na mastaa wengi wa tasnia hiyo, hakuna anayebisha kuwa marehemu Adam Kuambiana (alifariki dunia Mei 17, mwaka jana) alikuwa kichwa kwenye tasnia hiyo. Alifanya kazi na kampuni nyingi za kutengeneza sinema Bongo ikiwemo Jerusalem Films Productions chini ya JB. Kifo cha jamaa huyo kimeacha pengo kubwa.
Marehemu George Otieno ‘Tyson’ enzi za uhai wake.
TysonPia kifo cha George Otieno ‘Tyson’ aliyekuwa dairekta bora kabisa Bongo aliyefariki dunia Mei 30, mwaka jana, nacho kinatajwa kufifisha tasnia hiyo.Mbali na sinema za nyumbani, Tyson alifanya kazi kubwa kwenye michezo ya kuigiza ya runingani iliyosaidia kukuza tasnia hiyo Bongo.
Tatizo hili hawalioni!
Mbali na kuondoka kwa madairekta hao ambao kinachoonekana wengi wanaamini kuwa wameondoka na tasnia yao, lipo tatizo ambalo wengi hawalioni.Kwa sasa sehemu kubwa ya jamii yetu hainunui sinema za nyumbani kwa sababu wana chansi ya kuziona bure kupitia ving’amuzi.
Nini cha kufanya?
Kama walivyosema baadhi ya waigizaji kwenye makala haya, haina ubishi kwamba tasnia hiyo inaajiri vichwa vingi hivyo lazima jitihada zifanyike za kuinusuru.Ni vizuri waigizaji wakarejesha ule umoja wa Kaole Sanaa Group.Ni wakati muafaka wa kuweka pembeni majungu, visasi, bifu za kipuuzi, unafiki na wengine kujiona miungu watu kwani anguko tunalolishuhudia halibagui. Tunajenga nyumba moja, ya nini kugombea fito?
No comments:
Post a Comment