UCHAMBUZI WA SHERIA ZA MAKOSA MTANDAO, 2015
Awali
ya yote nirudie kutoa pongezi kwa serikali kwa hatua hii muhimu
waliyofikia ya kuwasilisha mswada wa sheria mtandao ambao naimani kubwa
itakua na majibu mazuri ya kudhibiti na kuhimili vishindo vya uhalifu
mtandao nchini. Naomba itambulike Tanznaia si ya kwanza kuwa na sheria
za usalama mitandao na ukweli ni kwamba tumechelewa kwa kiasi Fulani.
Nchi nyingi tayari zinasheria za usalama mitandao na zimeendelea
kuboreshwa kadri teknolojia inavyo endelea kukua na kubadilika.
Nitaanza
na mifano michache kunasheria mitandao zilizopendekeza kifungo cha
maisha kwa wahalifu mtandao nchini Uingereza. Na katika Kikao cha
usalama mitandao kilichopita mshiriki aliyekua nami meza kuu katika
kuongoza moja ya kikao aliyetokea “US Secret service” alipata kuainisha
adhabu ya miaka kumi na sita bado imeonekana ni ndogo na inashauriwa
kuongezwa makali.
Aidha,
Nieleze ushauri wa kuhakiki sheria mitandao zinaboreshwa na kuwa kali
zaidi ni kutokana na athari ya uhalifu mtandao kua kubwa sana na imekua
ikimgusa kila mmoja wetu – Kwan nje ya nchi kila siku tumekua tukipata
habari mpya ya matukio ya kiuhalifu mtandao ambapo maelfu wamekua
wakipoteza maisha, fedha na pia ufaragha wao umekua ukitumiwa vibaya na
wahalifu mtandao.
Tanzania
pia hatuko salama – Nimekua nikipata malalamiko mengi ya watu
kudukuliwa faragha zao, kuibiwa fedha nyingi sana na wengine kufikia
hata kujitoa maisha kwa kudalilisha mitandaoni.
Hayo
yote yamekua yakisukuma wataalam usalama mitandao kuumiza vichwa
kuhakiki wanakuja na mwarubaini wa uhalifu huu mtandao unaozidi kuota
mbawa kila kukicha. Hapo ndipo mengi yakawekwa sawa katika kukabiliana
na hali hii ikiwa ni pamoja na kukuza uelewa kwa watumiaji mtandao
(Matumizi salama ya mitandao), Kuzalisha na kuongezea uwezo kwa wataalam
wa usalama mitandao, kuwa na sharia stahiki za uhalifu mitandao, kukuza
ushirikiano kutokana na uhalifu huu kutokua na mipaka, kuhimiza
kupatikana kwa takwimu sahihi za uhalifu mitandao ili kuweza kutambua
maeneo athirika zaidi.
Kwenye
hili la Sheria ni hatua nzuri sana ambapo Tanzania imefikia ili kuweza
kurahisisha mapambano dhidi ya uhalifu mtandao nchini na kuhakiki taifa
linabaki salama kimtandao. Naimani Kila mmoja wetu ukizingatia wote ni
wahanga kwa namna moja au nyingine ya uhalifu mtandao lazima tufurahie
na kulipokea hili kwa mikono miwili. Wataalam wa usalama mitandao
wamefurahishwa sana na hatua hii yetu na pongezi ni nyingi sana hadi
sasa.
Kuondoa
hofu Watanzania naomba nieleze kwamba katika kuandaa muswada huu
wataalam na wadau mbali mbali walishirikishwa na badae kuvuka mipaka kwa
wataalam kutoka mataifa mbali mbali katika maswala haya ya usalama
mitandao kutoa maoni yao na kuboresha – Haikukomea hapo imepitia hatua
kadhaa na hata kupelekea kauli yangu niliyo itoa katika moja ya vikao
vya wataalam wa usalama mitandao kueleza kuwa “ Hatua za kitaalam
zimekwisha sasa ipo kwenye hatua za kisiasa kuweza kupatiwa Baraka kabla
ya kuwasilishwa bungeni” – Kauli ambayo wataalam
waliona taifa letu linachelewa sana kwani sharia zilikua hazina shaka na hata kupitiwa kwakwe kulipaswa kua kwa muda mfupi.
Nimepata
kufatilia kwa karibu kinachozungumzwa na wengi, Hofu kubwa nilizo ziona
ambazo nimeona nizitole ufafanuzi ni kama ifuatavyo: -
MOJA,
hofu kuwa uchunguzi wa makosa haya inaweza ikawa inakiuka faragha.
Naomba nieleze kuna anaefahamu faragha yake iko dhaifu kiasi gani mara
tu anavyo kua mtandaoni? Ni wazi kabisa unapaswa kujua faragha haiingi
matatani tu kwa sababu ya sharia hizi mtandao.
Uchunguzi
wowote wa uhalifu mitandao duniani kote unahusisha uangalizi wa kina
hatua kwa hatua kwa kila ushaidi wa kielektroniki ikiwa ni pamoja na
kupitia kwa karibu kila chembe ya shaka ya kile kinachoweza kuonekana
kinaweza kuwa na chembe ya sababu ya uhalifu mtandao.
Uchunguzi
wa makosa ya digitali ni fani na ina maadili yake – Maadili ambayo
yanasomewa darasani. Maadili hayo yana hakiki mchunguzi anafata masharti
na vigezo stahiki vya kimataifa ikiwa ni pamoja na kutotoa siri
zisizoendana na uhalifu mtandao unaochunguzwa pamoja na kuwasilisha
ushahidi kwa mhusika pekee bila kushirikisha kila mtu. Zaidi inawatu
maalum si kila mtu anatakiwa kushiriki katika uchunguzi wa uhalifu
mtandao. Na hili kuna moja ya masharti yana sisitiza kushirikisha idadi
ndogo sana ya wachunguzi ni vyema zaidi.
MBILI,
kuna hofu kwanini makosa mtandao yanapatiwa ruhusa ya kuchunguzwa bila
hata kusubiri ruhusa ya mahakama? Ikumbukwe kuwa kwanza uhalifu mtandao
unafanyika kwa haraka sana na hauna mipaka. Ndio maana hili limeangaliwa
sana na kuamua kutoa ruhusa kwa wapelelezi teule wa makosa ya uhalifu
mtandao kupewa fursa ya kuazisha uchunguzi mara moja bila ya kungoja
mahakama, Ikumbukwe kuna kinachoitwa “search warrant” ambacho mchunguzi
wa makosa mtandao anakua nacho nahii inatolewa na kiongozi katika
kitengo kinacho jihusisha na usalama mitandao katika taifa husika.
Kusisitiza hili kama pangetolewa ruhusa kusubiri protokali za mahakama
kufatwa kumbuka uhalifu mtandao unauwezekano mkubwa sana wa kupotezwa
ushaidi wake na kusababisha ugumu kwenye kufikia malengo.
TATU, Hofu
ya faragha ya kupekuliwa mawasiliano – Niulize kama unatumia mtandao
kuwasiliana vizuri hofu inatoka wapi kwenye hili. Kama unajua hunachembe
ya uhalifu mtandao katika mawasiliano yako sidahani kuna haja ya kua na
hofu kuchunguzwa. Na ikumbukwe yule aliyetiliwa mashaka pekee ndie
anaye pekuliwa si kila mmoja atapekuliwa mawasiliano yake. Hii iko kila
mahali duniani sisi sio wa kwanza.
Mimi
nadhani hofu kubwa tulitakiwa kuwa nayo ni kuhusu mamilioni ya pesa
yanayo potea katika mabenki yetu, athari za lugha za uchochezi kwenye
mitandao, athari za kuporomoka kwa maadili yetu, athari za mama na dada
zetu kusambazwa picha zao za uchi mitandaoni, athari za wasanii wetu
kutopata mapato kutokana na watu kuiba kazi zao mitandaoni, athari za
kudukuliwa na wahalifu mitandao na taarifa zetu kutumiwa vibaya, athari
za kuogopa kufanya miamala ya kifedha kupitia simu zetu, athari za
kuogopa kuweka pesa benki inayo pelekea uchumi wa taifa kuyumba, athari
zilizombele yetu zinazoweza kupelekea kuhatarisha maisha ( Kufa) kupitia
uhalifu mtandao na athari nyingine nyingi.
Ikumbukwe
athari ni kubwa sana za uhalifu mtandao na hofu kubwa tulipaswa tuwe
nayo na kwapamoja tuungane kuhakikisha sharia mtandao zinazidishwa
makali na uchunguzi wake unafanywa kwa kina na utaalam wa hali ya juu.
Hili ndilo linapelekea wataalam tunakutana mara kwa mara kuongezeana
uwezo wa kuhakiki tuna tambua mbinu mpya za uhali mtandao na kujinoa
kujua namna ya kuchunguza na kuweza kufikia malengo ya kudhibiti.
Wabunge
walionyesha hisia zao kutaka kupata ufumbuzi wa mabilioni ya pesa
yanayopotea katika mabenki na makampuni ya simu kupitia uhalifu mtandao –
Wanapaswa kukumbuka udhibiti unapaswa kwenda sambamba na kua na sheria
madhubuti zinazoweza kuhimili hali mbaya ya uhalifu mtandao nchini.
Naomba
tu kusisitiza watanznaia kusoma na kuelewa na sio tu kufata mikumbo
kwenye hili. Aidha, Hofu kubwa lazima iondoshe hofu ndogo. Nikiimanisha
Uhalifu mtandao nitishio kubwa kuliko ugaidi na sheria zetu zanafanana
kabisa na sheria nyingine za mataifa mbali mbali huku baadhi zikiwa kali
zaidi kuliko tulizo nazo.
Nimalizie
kwa kutoa wito wa matumizi salama ya mitandao ili kujiepusha na kuingia
matatani bila sababu za msingi. Huku nikiwatoa watanznaia hofu juu ya
uchunguzi wa dhati wa makosa haya uanafanywa na hakuana atakae ingia
matatani kama si muhusika.

No comments:
Post a Comment