TAASISI YA IMETOSHA FOUNDATIONS KUTUMA UJUMBE MZITO JIJINI MWANZA
Balozi Henry Mdimu akiongea na vyombo vya habari |
Taasisi isiyo ya ki serikali ya Imetosha Foundation
inayopinga unyanyapaa, ukatili na mauaji dhidi ya watu wenye ualbino
kwa njia ya elimu, inatarajia kutuma ujumbe mzito kanda ya ziwa hapo
kesho kwa maandalizi ya ujio wa timu nzima ya taasisi hiyo iliyojikita
kwenye kubadilisha mtazamo (mind set) wa watu juu ya janga hili. Ujumbe
huo utaongozwa na mwenyekiti wa taasisi hiyo Bw Masoud Kipanya, Balozi
Henry Mdimu Mgaya na katibu Salome Gregory,wajumbe watakaongozana na
viongozi hao ni pamoja na Mkala Fundikira, Isaya Mwakilasa (wakuvwanga
aka Baba Andunje) Zaytun Biboze, Kelvina John na msanii wa muziki wa
reggae Jhikoman Manyika.
Mwenyekiti Masoud Kipanya akiongea katika kilele cha matembezi ya hamasa yaliyofanyika jijini Dar |
Dhumuni
la safari hiyo itakayoupeleka ujumbe huo mpaka mkoani Shinyanga ni
kwenda kujitambulisha kwa viongozi wa serikali na usalama wa mikoa na za
kanda hiyo iliyoathiriwa sana na janga la ukatili na mauaji ya watu
wenye ualbino. Taasisi ya Imetosha imepanga kwenda kanda ya ziwa baadaye
mwezi ujao ambapo timu itaenda maeneo yaliyoathiriwa na kutoa elimu kwa
wakazi wa maeneo hayo kuwa si kweli kwamba ukiwa na kiungo cha mtu
mwenye ualbino utapata mafanikio, elimu hizo zitatolewa kwa njia ya
filamu mbali mbali, michezo ya kuigiza na matamasha ya muziki.
Hoteli ya Green Palm utakapofikia ujumbe wa Imetosha Foundation jijini Mwanza aka the Rock City. |
Ujumbe
huu ukiwa mjini Mwanza utakuwa chini ya udhamini wa hoteli ya Green
Palm iliypo maeneo ya Bwiru, vile vile kampuni ya Mwananchi
communication ltd (MCL) inayozalisha gazeti bora la Mwananchi na
mengineyo itachapisha habari zote kuhusiana na msafara huo wa Imetosha kanda ya ziwa. Meneja wa hotel .
Isaya Mwakilasa wa (Orijino komedi) Henry Mdimu na familia ya Isaya aka Wakuvwanga |
ya Green
Palm Bw Juma Herman ameuambia mtandao huu kuwa "imekuwa rahisi kwetu
(Green Palm Hotel) kudhamini makazi na usafiri kwa taasisi hiyo kwa kuwa
inachofanya ni kitu chema basi nasi tumeona ni vema tuwatie nguvu kwa
kuwapatia malazi na usafiri wa ndani kwa kipindi chote watakachokuwa
jijini Mwanza, kwa kweli sasa imetosha ukatili na mauaji dhidi ya watu
wenye ualbino" aliongeza.
Wakiongea
na mtandao huu kwa nyakati tofauti Mwenyekiti Masoud Kipanya na Balozi
Henry Mdimu walisema wanashukuru sana kwa kitendo cha Green Palm na
Mwananchi communictaion na kuwa ni vya kuigwa na makampuni mengine ili
kuiwezesha taasisi hiyo kufikia malengo yake. Taasisi ya Imetosha haina
vyanzo vya fedha hivyo kutegemea wahisani kama Green Palm Hotel na
Mwananchi communication.
Maktaba Baadhi ya wajumbe wa Imetosha wakijiandaa kwenda katika mchezo wa Simba na Yanga |
No comments:
Post a Comment