Shule ya sekondari ya Kutukutu Morogoro wafaidika na mradi wa "Airtel Shule Yetu"
Wanafunzi wa shule ya sekondari
Handeni iliyopo wilayani Handeni wakisoma vitabu vilivyotolewa na
Kampuni ya Airtel shuleni hapo kwa ajili ya masomo ya sayansi vyenye
thamani ya sh.milioni mbili.
Meneja
wa Mauzo wa Kampuni ya Simu za Mikononi ya Airtel Kanda,Aluta Kweka
kulia akimkabidhi Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Handeni Muhingo Rweymamu
vitabu vya masomo ya sayansi vilivyotolewa na kampuni hiyo vyenye
thamani ya sh.milioni mbili anayeshuhudia katikati ni Mwalikishi wa
Afisa Elimu wilaya ya Handeni,Ally Mwinyuma ambaye alimuwakilisha pia
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo.
Mwalimu
Mkuu wa shule ya Sekondari Handeni,Ally Adamu kulia akimkabidhi kitabu
mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo Aisha Juma cha Fizikia
ambavyo vilitolewa na kampuni ya simu za mikononi nchini Airtel vyenye
thamani ya sh.milioni mbili.
Uongozi
wa shule ya sekondari ya Kutukutu iliyopo wilayani kilosa mkoani
Morogoro, umeishukuru kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa msaada wa
vitabu vya masomo ya sayani.
Msaada
huo wenye thamani ya shilingi milioni mbili umekabidhiwa hivi karibu na
wawakilishi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ikiwa ni mpango wa
SHULE YETU unaosimamiwa na kampuni hiyo.
Akipokea
msaada huo kwa niaba ya walimu na wanafunzi wa shule hiyo mkuu wa shule
ya sekondari Kutukutu Finyilise Elias amesema, utasaida kuongeza ufaulu
wa wanafunzi wake wanaosomea masomo ya sayansi.
Mwalimu
Finyilise amesema, kumekuwa na ufaulu wa kusuasua kwa wanafunzi
wanaomaliza kidato cha nne hasa kwenye masomo ya sayansi hivyo msaada
huo utasaidia kuongeza ufaulu shuleni hapo. “ Wanafunzi wetu wanaosomea
michepuo ya sayansi wamekuwa na ufaulu mdogo sana na hii inatokana na
ukosefu wa vitabu vya masomo hayo kwa muda mrefu sasa” alisema Mwalimu
Mkuu huyo.
“msaada
huu utatusukuma haraka kwenye ufaulu wa kiwango cha juu wa masomo ya
sayansi kwani mwitikio wa wanafunzi wetu ni mkubwa na tunatarajia
tutapata matokeo ya haraka kutokana na msaada huu wa vitabu” aloingeza
Mwalimu Finyilise.
Awali
akikabidhi msaada wa vitabu hivyo, Meneja wa Airtel Mkoani Morogoro Bw.
Omar Bongo amesema, hatua hiyo ni kuwawezesha wanafunzi wa shule za
sekondari kupata maarifa ya masomo ya sayansi kwa vitendo. “Sisi wa
Airtel tumekuja hapa kusukuma gurudumu la maendeleo mbele kupitia elimu
na hasa vitabu vya kujifunzia, mkazo wetu kwa sasa ni masomo ya Sayansi
na tumeleta vitabu vya kujifunzia. Alisema Bw. Bongo.
Shule
hiyo ya sekondari kutukutu yenye wanafunzi zaidi ya 300 bado inakabiliwa
na changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na vyumba vya maabara na mazingira
mazuri ya kujifunzia
No comments:
Post a Comment