PDB YAKIRI KODI ZA BIASHARA SIZIZO RASMI HUISHIA KATIKA MIFUKO YA WATU NA SIO SERIKALI.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti ya Vyuo Vikuu vya Afrika ya Kati na
Kusini (ESAURP),Profesa Teddy Maliyamkono akifanya mahojiano mafupi na
Waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mkutano wa kuwajengea uwezo
sekta biashara zisizo rasmi iliofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu
Nyerere jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wadau na Wanahabari wakifuatilia mkutano wa uzinduzi wa mradi wa kuwajengea uwezo wajasiriamali wadogo na wakati kuhuisha biashara zao ili kupata huduma za kibenki iliofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Ufundi wa FSDT, Sosthenes Kewe alizungumza mbele ya wadau na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa mradi
wa kuwajengea uwezo wajasiriamali wadogo na wakati kuhuisha biashara
zao ili kupata huduma za kibenki,Bwa.Kewe amesema kuwa taasisi
yake imesaidia mradi huu kwa kuwa unaendana na kazi yao ya kuwezesha
wajasiriamali wadogo na wakati na hivyo kuchangia katika kukuza uchumi,
kutengeneza ajira na kupanua vyanzo vya kodi.
Mtendaji
Mkuu wa Ofisi ya Rais-Ufuatiliaji na Usimamizi wa Miradi (PDB),Omary
Issa akifanya mahojiano mafupi na Waandishi wa habari mara baada ya
kumaliza mkutano wa kuwajengea uwezo sekta biashara zisizo
rasimi iliofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es
Salaam.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
ZAIDI
ya biashara milioni tatu hazijasajiliwa na mamlaka za utambuzi wa
biashara hizo kutokana na kuwa mazingira magumu ya kusajili biashara
hizo ikichangiwa na rushwa.
Hayo
ameyasema Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Rais-Ufuatiliaji na Usimamizi wa
Miradi (PDB),Omary Issa wakati mkutano wa kuwajengea uwezo sekta ya
biashara isiyo rasmi, uliofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere
jijini Dar es Salaam.
Issa
amesema wajasirimali wamekuwa wakilipa kodi lakini zinaishia katika
mifuko ya watu na kuisababishia serikali kukosa mapato. Amesema
wajasiriamali wakirasimishwa katika mpango huu wataongeza mapato kuliko
ilivyo sasa kwa kulipa watu wanaoingiza mifukoni mwao na kuacha
serikali kukosa kodi hizo.
Aidha
amesema asilimia 40 ya biashara ndogo hazijasajiliwa na mamlaka
zinahusika na kufanya wajasiriamali hao kushindwa kupata mikopo katika
taasisi za kifedha.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti ya Vyuo Vikuu vya Afrika ya
Kati na Kusini (ESAURP),Profesa Teddy Maliyamkono amesema mradi huu wa
kurasimimisha biashara utasaidia kukua biashara zao.
Amesema
watu wamekuwa wakifanya biashara hazikui kutokana na mitaji yao kuwa
midogo na kukosa fursa kukopa katika taasisi za fedha.
No comments:
Post a Comment