MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI KUTOKA AFRIKA KUSINI REBECCA MALOPE AWASILI USIKU HUU KUTUMBUIZA KESHO TAMASHA LA PASAKA JIJINI DAR.

Mwimbaji
wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini anayetambulika kwa jina
la Rebecca Malope akipungia mkono mashabiki wake hawapo pichani mara
baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius
Kambarage Nyerere (JNIA) jioni hii tayari kwa kutumbuiza katika tamasha
la miaka 15 ya Tamasha la Pasaka linalofanyika kesho kwenye uwanja wa
michezo wa Taifa jijini Dar es salaam, ambapo Solly Mahlangu mwanamuziki
nguli mwingine wa muziki wa injili kutoka nchini humo atawasili kesho
na kujiunga moja kwa moja na tamasha hilo.Kulia ni Alex Msama Mkurugenzi
wa kampuni ya Msama Promotion.
Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini anayetambulika kwa jina la Rebecca Malope akivishwa skafu ya bendera ya Taifa ya Tanzania na mmoja wa maofisa wa kampuni ya Msama Promotion Bi Nyakwesi.
Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini Rebecca Malope akizungumza
na vyombo vya habari mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa
Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku huu tayari kwa kutumbuiza
kesho kwenye tamasha pa Pasaka.Kuklia kwake ni Mkurugenzi wa Msama
Promotions Ltd,Bwana.Alex Msama akitabasamu.
Rebecca Malope akifurahia kutua tena nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment