MASHINE ZA BVR AWAMU YA PILI KUPELEKWA MIKOA SABA
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi Nchini Tanzania itaanza kusambaza mashine za BVR
248 katika mikoa saba nchni Tanzania Kuanzia katikati mwa wiki ijayo.
Mikoa
iliyopangwa kuanza kupokea mashine hizi ni mikoa ya Lindi, Mtwara,
Ruvuma, Iringa, Wakati zozi likianza mikoa hiyo nyingine zitakuwa
zinapelekwa katika mikoa ya Katavi, Mbeya na Dodoma. Mikoa mimgine ni
Singida Tabora Geita na Kigoma.
Mkuu wa kitengo cha Ufundi wa idara ya Daftrari/ICT wa NEC Dr Sisit Cariah, Akizungumza na mwandishi wetu amesema kwamba mpaka sasa wanachi wa mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvumna na Iringa wakae tayari kwani muda wowote watatangaziwa vituo vya kujiandikisha.

Pamoja
na mshine hizo 248 Tume ya taifa ya uchaguzi imewaandaa wataalamu 248
ambao watakuwa na jukumu la kutoa elimu kwa wataalamu wengine 50 kwa
kila mmoja nchi nzima kwa ajili ya kuharakisha uandikishaji kwa mfumo wa
BVR.
Dr
Sisit Ameeleza kwamba wamefanikiwa kufanya maboresho makubwa katika
mashine hizi ikiwa ni pamoja na kubadilisha upangaji wa vifaa
(settings), mfumo endeshi (Software) na upande wa Vichapishio (printer)
ambazo sasa zimetengenezewa Nchini Ufaransa umeboreshwa na nirahisi
kusafishwa.
Mafunzo
yaliyoendeshwa hapa Jijini Dar es Salaam yamechukua siku moja na
yamezingatia sana upande wa Vichapishio (printer), Visoma alama za
vidole (Finger Print Scaner) na Kamera kutambua macho mekundu. Ameongoza
kwamba printer za sasa ni rahisi kusafishwa na hata kuweka kifaa kipya
baada ya cha zamamni kuharibika vimerahisishwa.
Kuhusu
uchukuaji wa alama za vidole, amesema kwamba kwa sasa tatitzo la
mashine ya kuchukua alama za vidole wamelifanikisha kwa asilimia mia.
Kwani kwa wale ambao hawana alama za vidole mashine zimewekewa mfumo wa
alogarithim mpya ambao uatatambua kila aina ya kidole.
Hata
hivyo Kamera zimewekewa mfumo mpya wa kutambua macho mekundu na
kurekebisha rangi ya macho mekundu (Red eyes) Bila kukwamisha zoezi la
uandikishaji.
Mtarajio
ni kwamba zoezi lauandikishaji liwe limekamilika ndani ya kila siku 28
tokea kila mkoa unapopokea mashine hizi. Vilevile Dr Sisit ameishukuru
serekali kwa kufanikisha upatikanaji wa Vifaa “serekali imejitahidi
kuandaa upatikanaji wa mashine hizo, na usafirishaji kwa njia ya ndege
kwenda nchi nzima.
Kila halmashauri na mkoa utachukua angalau siku 28 kukamilisha mkoa utakapo pokea Vifaa” Dr Sisit amesema.Mwisho amesema kwamba mashine nyingine 1,600 zitawasili wakati wowote na kwamba serikali imetoa Dola za Marekani milioni 72 (Sh. bilioni 133).

Kuwasili
kwa mashine hizo, kunaifanya Nec kupokea mashine 2,098, huku ikisubiri
mashine 5,902, ili kukamilisha 8,000 zinazotakiwa. Alisema vifaa hivyo
vinanunuliwa na serikali kupitia kampuni ya Lithotech Export ya Afrika
Kusini, ambayo imeingia mkataba na Nec na inaviagiza China.
No comments:
Post a Comment