Marufuku Kupiga Kelele Tanzania
Na victor Mariki – Ofisi ya Makamu wa Rais.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Maku wa Rais - Mazingira, Mh. Binilith Mahenge,
amezindua Kanuni mpya ya Mazingira itakayodhibiti uchafuzi wa mazingira
unaotokana na makelele yanayosabishwa na shughuli mbalimbali katika
jamii .
Akizungumza
katika uzinduzi wa Kanuni hizo jijini Dar es Salaam, Mh. Mahenge
alisema kuwa Ofisi yake ilishazitangaza Kanuni hizo katika Gazeti la
Serikali tangu tarehe 30/01/2015 kulingana na Sheria ya Usimazi wa
Mazingira ya mwaka 20104.
Aidha
Mh. Mahenge aliongeza kuwa Sheria hiyo ya Mazingira ya mwaka 2004
iliyoanza kutumika rasmi tarehe 1 Julai, 2015 inaiwezesha Ofisi yake
kuandaa na kuunda kanuni mbalimbali za mazingira ili kudhibiti uchafuzi
wa mazingira nchini.
Hata
hivyo alifafanua kuwa kanuni mpya za kudhibiti kelele, hazitadhibiti
kelele zitokanazo na ving`ora vya magari ya Polisi, magari ya zimamoto,
magari ya kubebea wagonjwa pamoja na mizinga wakati wa magwaride katika
sherehe za kitaifa.
Kanuni
hizi zimeundwa kuitikia wito wa malalako kuotoka kwa wadau mbalimbali
waliokuwa wakiilalamikia serikali kuhusu uchafuzi mkubwa wa mazingira
unaotokana na kelele katika kumbi za starehe, uchmbaji wa madini pamoja
namitetemo inayosabishwa na minara ya simu
No comments:
Post a Comment