Huawei kushirikiana na mataifa ya Afrika kuboresha mawasiliano
Baadhi
ya washiriki wa mkutano wa masuala ya Ugunduzi wa Digitali Afrika wa
mwaka 2015 'Innovation Africa Digital (IAD) uliyofanyika nchini Zimbabwe
ambapo Huawei ikiwa mshiriki iliahidi kushirikiana na nchi za Afrika
katika kukuza sekta ya Teknohama.
KAMPUNI
nguli katika sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano ya Huawei
imeomba uwepo wa ushirikiano baina yake na mataifa ya Afrika hususani
katika nyanja za teknolojia ya habari na mawasiliano (TEKNOHAMA).
Kwa
mujibu wa Makamu wa Raisi wa kampuni hiyo katika ukanda wa Mashariki na
Kusini Bw David Wang, hatua hiyo inalenga kutimiza adhma ya pamoja baina
ya kampuni hiyo na mataifa ya Afrika katika kuunganisha bara hilo
katika mfumo wa mawasiliano.
“ Ili
kufanikisha adhma hii ya kuunganisha bara hili katika mfumo wa
mawasiliano, Huawei tunategemea zaidi ushirikiano kutoka kwenye serikali
za mataifa ya Afrika,’’ alisema Bw Wang kwenye Mkutano wa mwaka wa
masuala ya uvumbuzi wa digitali (IAD) uliofanyika
mjini Victoria Falls, Zimbabwe hivi karibuni.
Kama
mdau maalumu kwenye mkutano huo, kampuni hiyo ilipata fursa ya kuonyesha
uvummbuzi wake kwenye masuala ya TEKNOHAMA pamoja na vifaa vyake. Kwa
mujibu wa Bw Wang, ili kuenda sambamba na kaulimbiu
'UpatikanajiNafuu’ ya mkutano huo , Huawei kwa sasa wanatengeneza
mtandao wa miundombinu ya mawasiliano, ikiwemo mitandao wa LTE kwa ajili
ya taifa laZimbabwe.
Mradi
huo unalenga kuziba pengo la maendeleo ya kidigitali kwa kuongeza eneo
linalofikiwa na mtandao wa mawasiliono nchini humo pamoja na huduma kwa
bei nafuu. “Lakini pia kwenye hili vipaji vya TEKNOHAMA ni muhimu sana
kwa maendeleo ya bara hili. Huawei inajikita zaidi pia kwenye kuandaa
vipaji hivi kwenye bara hili.’’ Alisema
Akielezea
zaidi Bw Wang alisema mnamo mwezi Oktoba mwaka huu Huawei kwa
kushirikiana na Serikali ya Zimbabwe watatekeleza mpango wa kijamii wa
kampuni hiyo uitwao “Mbegu kwa ajili ya baadae’ utakaotoa fursa kwa
wanafunzi 10 kutoka nchini humo kupata mafunzo ya TEKNOHAMA katika makao
makuu ya kampuni hiyo nchini China.
Akizungumza kwenye Mkutano huo, Waziri wa TEKNOHAMA, Posta nahuduma za usafirishaji nchini Zimbabwe Bw.
Supa Mandiwanzira alionyesha kutambua kampuni ya Huawei kama nguli wa
masuala ya TEKNOHAMA ulimwenguni na yenye utaalamu na
uzoefu kiutandawazi katika kutoa hudumanafuu za masuala ya TEKNOHAMA
nchini humo.
Mkutano huo wa siku mbili (kutoka Aprili 14-16)ulihusisha washiriki 500,wakiwamo
watunga sera, mashirka simamizi, watoa huduma na watumiaji wa kuu wa
TECNOHAMA kutoka Afrika na sehemu nyingine dunia, kwa lengo la
kutoa huduma muhimu kwa wanahisa , ili kuboresha mazingira ya teknolijia
hiyo na kukuza maendeleo ya sekta hiyo.
No comments:
Post a Comment