Header Ads

WAZIRI WA FEDHA MHE. SAADA SALUM MKUYA AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA BENKI YA DUNIA KANDA YA AFRIKA

SAD6Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia ukanda wa Afrika Bw. Makhatar Diop na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier,wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya alipokuwa akitoa msimamo wa Tanzania katika mkutano huo uliofanyika mjini Washington DC.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akipiga mahesabu ya haraka haraka na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile, baada ya kuulizwa swali na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia ukanda wa Afrika Bw. Makhatar Diop,( hayupo kwenye picha).Kulia ni Bw. Rished Bade Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania na kushoto ni Gavana msaidizi wa Benki kuu ya Tanzania Bi. Natu Mwamba.
sad2Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia ukanda wa Afrika Bw. Makhatar Diop pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier wakitafuta kitu cha kumuuliza Waziri wa fedha (hayupo kwenye picha)katika mkutano uliofanyika mjini Washington DC.
sad3Ujumbe wa Mkutano huo kutoka pande zote mbili yaani Tanzania na Benki ya Dunia, wakiwaangalia wajumbe waliokuwa wakijitambulisha.sad4Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akijibu maswali aliyokuwa akiulizwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia ukanda wa Afrika Bw. Makhatar Diop aliyeko mbeleyake.Kulia kwa Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile akifuatiwa na Bw. Rished Bade Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania.
sad5Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akijibu maswali aliyokuwa akiulizwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia ukanda wa Afrika Bw. Makhatar Diop aliyeko mbeleyake.Kulia kwa Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile akifuatiwa na Bw. Rished Bade Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania.
Picha zote na Ingiahedi C. Mduma – Washington DC.

No comments:

Powered by Blogger.