ZIARA YA KIKAZI YA BODI YA USHAURI YA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII (MAB) KWA TFDA JIJINI ARUSHA
Utendaji wa TFDA Katika Udhibiti wa Bidhaa Za Vyakula, Dawa, Vipodozi na Vifaa Tiba Wapongezwa.
Katibu
Tawala (RAS) wa Mkoa wa Arusha, Bw. Adon S. Mapunda, akiwakaribisha
wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa TFDA
(MAB) wakati walipofanya ziara ofisini kwake mapema wiki hii kwa lengo
la kujadili mikakati ya kudhibiti chakula, dawa na vipodozi mkoani
Arusha. Pamoja na mambo mengine, Bw. Mapunda aliipongeza TFDA kwa utendaji kazi mzuri na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika kulinda afya ya jamii. Kushoto ni Mwenyekiti wa MAB, Balozi Dkt. Ben Moses na anayesaini kitabu cha wageni ni Mkurugenzi Mkuu wa TFDA na Katibu wa MAB, Bw. Hiiti Sillo. 
Mkurugenzi
Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti Sillo, akisisitiza jambo wakati wa kikao na
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha kuhusu utendaji kazi wa TFDA Kanda ya
Kaskazini wakati wa ziara ya Wajumbe wa MAB na Menejimenti ya TFDA Ofisini kwa RAS mapema wiki hii. Wengine katika picha ni wajumbe wa
MAB na Menejimenti ya TFDA.
Mkurugenzi
wa Jiji la Arusha, Bw. Juma Iddi, akimsikiliza Mwenyekiti wa MAB
Balozi Dkt. Ben Moses (aliye kulia kwake) wakati wajumbe wa Bodi hiyo
walipofanya ziara ofisini kwake mapema wiki hii kwa lengo la kujadili
mikakati ya kudhibiti chakula, dawa na vipodozi mkoani Arusha. 
Mwenyekiti
wa MAB, Balozi Dkt. Ben Moses, akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Bodi
hiyo wakati wa kikao cha kujadili mikakati mbalimbali ya utendaji kazi
wa TFDA kilichofanyika katika ofisi ya TFDA Kanda ya Kaskazini Jijini
Arusha mapema wiki hii
No comments:
Post a Comment