KINANA AITIKISA ARUSHA,AVUNA WANACHAMA WAPYA ZAIDI YA 4000 WAKIWEMO VIGOGO WA CHADEMA.
Aliyekuwa
Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Monduli,Amani Ole Torongei,akizungumza
jambo mbele ya umati wa watu waliofika katika mkutano wa hadhara
uliofanyika jioni ya leo huku akionesha fulana ya CHADEMA akieleza kuwa
amechoka kuwa mtumwa.Amani alitangaza kukihama chama chake na kutangaza
rasmi kuhamia chama cha CCM,ambapo pia alikabidhi kadi yake ya awali kwa
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na kukabidhiwa kadi mpya ya chama hicho
cha CCM.
Aliyekuwa
Mwenyekiti wa wilaya ya Ngorongoro kupitia chama cha CHADEMA,Revocatus
Mpalampala,akizungumza jambo mbele ya umati wa watu waliofika katika
mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo.Revocatusi alitangaza
kukihama chama chake na kutangaza rasmi kuhamia chama cha CCM,ambapo pia
alikabidhi kadi yake ya awali kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na
kukabidhiwa kadi idhi kadi yake ya awali kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na kukabidhiwa kadi mpya ya chama hicho cha CCM.
Aliyekuwa
Katibu Mwenezi Kata ya Olorien,mkoani Arusha kupitiaa chama cha
CHADEMA,Prosper Mfinanga akivua sare za chama chake kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika jioni ya leo,akiashiria kukihama chama hicho na
kuhamia chama cha CCM,ambapo pia alikabidhi kadi yake ya awali kwa
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na kukabidhiwa kadi mpya ya chama hivyo.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa mji wa
Arusha na vitongoji vyake katka mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya
leo katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.Ndugu Kinana akiwa
emeambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na wajumbe
wengine leo wanahitimisha ziara ya siku nane mkoani humo ya
Kuhimiza,kukagua na kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010
ikiwemo sambamba na kusikiliza matatizo ya wananchi na kuyatafutia
ufumbuzi.
Ndugu
Kinana katika ziara yake ndani ya mkoa wa Arusha ametembea umbali wa
kilometa 2671,Wilaya zote sita za mkoa huo yakiwemo na majimbo saba ya
uchaguzi.Amefanya mikutano 69,mikutano nane ya ndani na mikutano 61 ya
nje kwa kuzungumza na Wanachi kuyasikiliza matatizo yao na kuyatafutia
ufumbuzi.Kama vile haitoshi Ndugu Kinana ametembelea miradi 49,miradi
sita ya CCM katika kutekeleza Ilani ya uchaguzi na miradi 43 ya
serikali.
Katika
taarifu fupi ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi kuhusiana na wanachama
wapya,ziara hiyo imejiongezea wanachama wapya wapatao 4290,ambapo
wanachama 519 kutoka CHADEMA walijiunga na chama hicho cha CCM.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Arusha
waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika
uwanja wa Sheikh Amri Abeid jioni ya leo.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia mkutano huo.
Baadhi
ya wananchi wakifuatilia mkutano huo,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
Kinana alipowahutubia jioni ya leo katika uwanja wa Sheikh Amri
Abeid,wakati wa kuhitmisha zaira yake ya siku nane ndani ya mkoa huo.
Baadhi ya Wafuasi wa chama CCM wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo wa hadhara.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikabidhiwa ngao ya heshima kutoka kwa
Mwenyekiti wa Vijana wa CCM mkoa wa Arusha,Bwa.Robinson Meitinyiku.
Aliyekuwa
Katibu Mwenezi Kata ya Olorien,mkoani Arusha kupitiaa chama cha
CHADEMA,Prosper Mfinanga akikabidhi kadi yake ya CHADEMA kwa Katibu Mkuu
wa CCM,Ndugu Kinana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia mkutano huo.
Wananchi na wafuasi wa CCM wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo
Aliyekuwa
Katibu Mwenezi Kata ya Olorien,mkoani Arusha kupitia chama cha
CHADEMA,Prosper Mfinanga akivua sare za chama chake kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika jioni ya leo,akiashiria kukihama chama hicho na
kuhamia chama cha CCM,ambapo pia alikabidhi kadi yake ya awali kwa
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na kukabidhiwa kadi mpya ya chama hivyo.
Gwanda la Proper likipepea hewani mara baada ya kuvuliwa na kutupwa kule.
Magwanda ya CHADEMA yakiwa yamekusanywa na wafuasi wake kuhamia chama cha CCM.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wananchi katika mkutano huo
Sehemu
ya umati wa wakazi wa mji wa Arusha waliojotokeza kwa wingi kusikiliza
hotuba ya katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowahutubia jioni ya leo
jijini Arusha.
No comments:
Post a Comment