MAANDALIZI YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO-MAAFISA NA ASKARI WA JESHI LA MAGEREZA
Baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza
wakiwa katika mazoezi ya kukimbia katika viunga vya manispaa ya Moshi
ikiwa ni maandalizi ya kupanda mlima Kilimanjaro March 6, 2015. Maafisa
hao
wameweka kambi katika eneo la Gereza Karanga-Moshi.
Baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza
wakiwa katika mazoezi ya kutembea katika viunga vya Manispaa ya
Moshi ikiwa ni maandalizi ya kupanda mlima Kilimanjaro mnamo Machi 6,
2015. Kutoka kushoto ni Mkaguzi wa Magereza Vicent Magessa kutoka Gereza
Bagamoyo Mkoa wa Pwani, Mkaguzi wa Magereza Tumaini Kihampa na Mkaguzi
wa Magereza Jamhuri Yassin wote kutoka Makao Makuu ya Magereza.
Sehemu ya Maafisa na Askari wa Jeshi
la Magereza wakiwa katika mazoezi makali katika mitaa ya mji wa
Moshi ikiwa ni maandalizi ya kupanda mlima Kilimanjaro ifikapo Machi
6,2015. Katikati (mwenye vazi jeupe) ni Kamishna Msaidizi wa Magereza
Alexander Mmasy kutoka Makao Makuu ya Magereza, wa kwanza kulia ni Mrakibu
Msaidizi wa Magereza Mbezi Ramadhani kutoka Ofisi ya Mkuu wa Magereza
Mkoa wa Tanga na wa kwanza kushoto ni Mkaguzi wa Magereza Jamhuri Yassin
kutoka Makao Makuu ya Magereza, Dar es salaam.
Baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la
Magereza wakiwa katika mazoezi ya viungo baada ya kutembea na
kukimbia katika viunga vya Manispaa ya Moshi ikiwa ni maandalizi ya
kupanda mlima Kilimanjaro mnamo Machi 6, 2015.
No comments:
Post a Comment