 |
| Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi
Juma Maalim (Mb.) akizungumza na Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti kwenye
Kundi la Wataalam chini ya Umoja wa Mataifa linaloshirikisha wadau
kutoka sekta ya umma na binafsi kukabiliana na Mabadiliko ya
Tabianchi-Intergovernmental Panel on Climate Change-IPCC, Prof.
Jean-Pascal Van Ypersele kutoka Ubelgiji ambaye alifika Wizarani kwa
ajili ya kumsalimia Mhe. Maalim. Katika mazungumzo yao Prof. Ypersele
alielezea dhamira yake ya kushirikiana na nchi zinazoendelea katika
kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuongeza wataalam kwenye
kundi hilo pindi atakapochaguliwa kwenye nafasi hiyo. |
 |
| Prof. Ypersele nae akichangia jambo wakati wa mazungumzo yao. Kushoto ni Balozi wa Ubelgiji hapa nchini, Mhe. Koenraad. |
 |
No comments:
Post a Comment