Header Ads

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AANZA ZIARA YAKE WILAYANI MPWAPWA MKOANI DODOMA LEO.


 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa Mpwapwa mapema leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Mashujaa mjini Mpwapwa.Kinana ameanza ziara ya siku 9 mkoani Dodoma ya Kuiarisha uhai wa chama,kukagua,kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2010 pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
  Baadhi ya Wananchi na wanachama wa CCM,wakishangilia jambo walipokuwa wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia katika uwanja wa Mashujaa,wilayani Mpwapwa leo jioni 
 Baadhi ya Wananchi na wanachama wa CCM,wakishangilia jambo walipokuwa wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana  alipokuwa akiwahutubia katika uwanja wa Mashujaa,wilayani Mpwapwa leo jioni 
Wakazi wa Mpwapwa wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mapema leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Mpwapwa
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi-Taifa,Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Mpwapwa mapema leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Mashujaa mjini Mpwapwa mkoani Dodoma.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Berege,wilaya ya Mpwapwa.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki ujenzi wa mifereji
 ya umwagiliaji katika shamba la Umwagiliaji katika kijiji cha Msagali kata ya Chunyu.Kinana alikagua na kushiriki ujenzi wa ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji skimu ya Msagali
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa sambamba na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma,Mh.Adam Kimbisa wakishiriki ujenzi wa Zahanati katika kijiji cha Kisoke,Wilaya ya Mpwapwa,mkoani Dodoma
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizindua na kushiriki ujenzi wa ofisi ya tawi la CCM wilaya ya Mpwapwa.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikatiza kwenye moja ya
mtaro alipokwenda kukagua na kushiriki kulima katika shamba la mkulima bora wa mwaka 2014,Bi.Anna Mlewa katika kijiji cha Berege,wilaya ya Mpwapwa.
 Sehemu ya ujenzi na ukarabati wa mfereji wa umwagiliaji
 Pichani Kati ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameongoza na Mkulima bora wa mwaka 2014,Bi.Anna Mlewa na Mumewe pichani kulia,ambapo Ndugu Kinana alikwenda kukagua na kushiriki kulima katika shamba la mkulima huyo katika kijiji cha Berege,wilaya ya Mpwapwa.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (wa tatu kushoto) akishiriki kulima shamba la karanga la Mkulima bora wa mwaka 2014 mkoa wa Dodoma,Bi.Anna Mlewaka katika kijiji cha Berege Wilayni Mpwapwa mkoani Dodoma.Mkulima huyo alieleza mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kuwa 2012/13 alifanikiwa kulima ekari 30 na kuzalisha kiasi cha gunia 300 za mtama,mnamo mwaka 2014 alihamasika kuongeza eneo kufikia ekari 130 ambazo alizalisha gunia 650.Mkulima huyo alisema kuwa mpaka sasa amefanikiwa kununua power tiller 1,ameanzisha biashara ya duka na mashine ya kusaga,anasomesha watoto shule ya msingi,sekondari na chuo.

No comments:

Powered by Blogger.