KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YAFANYA UKAGUZI KWENYE VITUO VYA KUPOOZA NA KUSAMBAZA UMEME KATIKA MIKOA YA ARUSHA NA KILIMANJARO
Mjumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambaye ni Mbunge wa
Viti Maalum Jimbo la Singida, Martha Mlata (kushoto) akisalimiana na
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco)
Dkt. Miganda Manyahi (kulia), jijini Arusha kabla ya kuanza kwa ziara
kwenye miradi ya umeme. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini
inafanya ziara katika miradi ya umeme iliyopo katika mikoa ya Arusha
na Kilimanjaro ili kujionea hatua ya utekelezwaji wake pamoja na
kuzungumza na watendaji.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Daudi Felix Ntibenda ( wa nne kutoka kushoto
waliosimama mbele), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati
na Madini Richard Ndassa ( wa tano kutoka kushoto waliosimama mbele)
wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Nishati na Madini na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini
mara baada ya kumalizika kwa kikao.
Meneja
Mradi wa Kusambaza Umeme unaojulikana kwa jina la Electricity V
unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Mhandisi Florence
Gwang’ombe
(kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Nishati na Madini Richard Ndassa (kulia) mara baada ya kamati
hiyo kuwasili kwenye eneo la mradi huo ili kujionea maendeleo ya
utekelezwaji wake.
Mtaalam
kutoka Kampuni ya Sweco International AB, Pal Aberg (kushoto)
akiielezea Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini hatua
iliyofikiwa ya ujenzi wa kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha Njiro
kilichopo nje kidogo ya jiji la Arusha.
Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ikiendelea na ziara katika
eneo la kituo cha kupooza na kusambaza umeme kilichopo Njiro nje kidogo
ya jiji la Arusha.
No comments:
Post a Comment