Header Ads

Gharama za kuunganisha umeme shilingi 177,000. Atakayetoza zaidi ya hapo kufikishwa polisi - Ndassa


 Meneja Miradi kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Khalid James (kulia) akiieleza Kamati ya   Bunge ya Nishati na Madini  hatua iliyofikiwa ya   ujenzi wa miundombinu  ya umeme katika   mikoa ya  Iringa, Dodoma,  Singida hadi   Shinyanga inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili. Kamati ya  Bunge inafanya ziara katika  mikoa  ya Dodoma, Singida, Arusha na  Kilimanjaro  kwa  ajili ya
kukagua miradi ya umeme   ili kujionea maendeleo  yake pamoja na kuzungumza na wananchi
 Meneja Miradi kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Khalid James (katikati) akitoa maelezo  mbele ya Kamati ya  Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu  maendeleo ya ujenzi wa njia kuu za umeme unaofanywa  na kampuni ya Jyoti Structures Limited kutoka India katika eneo la Nara mkoani Dodoma
Moja ya mrara kwa ajili ya njia  kuu ya umeme  ikiwa chini ya ujenzi  unaosimamiwa na kampuni ya Jyoti Structures Limited kutoka India. Nguzo moja inagharimu  shilingi  milioni 200.

No comments:

Powered by Blogger.