CCM YATOA TAMKO KUFUATIA TUHUMA ZA KUTAKA KUWAWA KWA KATIBU MKUU WA CHADEMA,DKT SLAA.

Tarehe
08/03/2015, Dr. Wilbroad Slaa Katibu Mkuu wa Chadema kupitia kwa mjumbe
wa Kamati Kuu ya Chadema Ndugu Mabere Marando alitoa tuhuma kwa
Serikali na kuwahusisha baadhi ya viongozi wa juu wa CCM kuwa wanapanga
njama za kumdhuru Katibu Mkuu huyo wa Chadema.
Kimsingi tuhuma hizi ni za
kipuuzi, lakini uongo huu usipojibiwa unaweza kugeuzwa kuwa ajenda na
Chama hiki cha Chadema kwa kukosa ajenda zingine za maana. Hakuna
asiyejua kuwa Chadema kwa sasa kinapumulia mashine, hivyo maneno na
matendo yao kwa sasa lazima yalenge kujaribu kujinasua na balaa la kufa
kwa chama chao.
Ni vizuri Watanzania wakakumbuka
historia ya tuhuma lukuki zilizowahi kutolewa na Katibu Mkuu huyu wa
Chadema toka aanze siasa na ambazo zote zilikuja thibitika kuwa ni za
uongo. Hapa nitawakumbusha baadhi.
Akiwa Singida katika kampeni za
Urais za mwaka 2010, Dk. Slaa aliwatangazia wananchi mkutanoni kwamba
kulikuwa kumekamatwa lori kubwa la mizigo (semi-trela) lililojazwa
karatasi za kura za Urais zilizokuwa tayari amepigiwa kabisa mgombea
Urais wa CCM, Dk. Jakaya Kikwete.
Katika kuonyesha kwamba alikuwa na
uhakika wa jambo hilo, alisoma hadi namba za lori hilo na tela lake
kutoka kwenye karatasi aliyokuwa ameshika mkononi, kisha akasema kuwa
lori hilo lilikamatwa katika mji mdogo wa Tunduma, mkoa wa Mbeya wakati
likiingia nchini kutoka Lusaka, Zambia.
Lakini baada ya polisi kuchukua
hatua za haraka wakitumia namba za lori na tela lake alizokuwa amezisoma
na kulikamata, kisha wakalipekua hadharani huku wananchi wakishuhudia
palepale Tunduma, kilichokutwa ndani ya lori ilikuwa shehena ya vipodozi
vya kina mama na sabuni za manukato.
Baada ya siku chache huku akiwa
amesahau yote, Dk. Slaa akatangaza tena kuwa mgombea Urais wa CCM, Rais
Jakaya Kikwete alikesha katika hoteli ya Lakairo, Mwanza akiweka
mikakati ya kuiba kura siku ya uchaguzi huo wa mwaka 2010 ili ashinde.
Siku chache alisema kura zimeingizwa na zimeshapigwa, hapa amesahau
anadai ndio kwanza mpango unapangwa.
Aliwataja watu wengine aliodai
walikuwa pamoja na Rais Kikwete kuwa ni aliyekuwa Mbunge wa Igunga,
Rostam Aziz na Mkurugenzi wa Hoteli hiyo iliyopo katika jiji la Mwanza,
Lameck Airo. Lakini wakati Dk. Slaa akisema
uongo huo, Rais Kikwete siku nzima na usiku wake wote alikuwa Mtwara
akiendelea na kampeni zake za Urais.
No comments:
Post a Comment