Header Ads

Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo Tundu Lissu ametangaza kuvuliwa rasmi uanachama wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe.


 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe
Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu 
---  
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini,  Zuberi Zitto Kabwe, amevuliwa uanachama wake mchana huu katika ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jijini Dar es Salaam katika hatua iliyotangazwa na mnadhimu mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu, baada ya mbunge huyo kushindwa kesi iliyokuwa amefungua katika Mahakama Kuu ya Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi hizo, Lissu alisema Zitto amefutwa uanachama  kwa mujibu wa taratibu na sheria ya chama isemayo  kwamba endapo mwanachama atapata tatizo lolote binafsi ama la kichama, malalamiko yote yatasuluhishwa ndani ya chama na si mahakamani

“Hivyo,  kwa mujibu wa sheria za chama, Zitto alikiuka sheria  anapaswa kuvuliwa uanachama wake,” alisema Lissu.

No comments:

Powered by Blogger.