TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAKUTANA NA VIONGOZI WA SIASA JIJINI DAR LEO.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Damian
Lubuva
akizungumza wakati wa mkutano na Viongozi wa Vyama vya Siasa
uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa JB Belmonte,Jijini Dar es
salaam.Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Julius
Malaba na kulia ni Kamishina wa Tume yaTaifa ya Uchaguzi,Prof. Amon
Challigha

Sehemu
ya Viongozi wa Vyama vya Siasa waliohudhulia Mkutano huo wakimsikiliza
kwa makini Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Damian
Lubuva (hayupo pichani) leo kwenye Ukumbi wa JB Belmonte,Jijini Dar es
salaam.

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini,Jaji Francis Mutungi akichangia
mada katika mkutano huo wa Viongozi wa Vyama vya Siasa uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa JB Belmonte,Jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti
wa Chama cha UDP,Mh. John Momose Cheyo akiwa na Katibu wa NEC,Itikadi
na Uenezi CCM,Ndg. Nape Nnauye wakati wa mapumziko mafupi ya mkutano
huo.

Mwenyekiti wa CHADEMA,Mh. Freeman Mbowe akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Chama cha ACT,Ndg. Samson Mwigamba.

Eeehh....bwanaaaaa
upoooo........?? Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi,Mh. James Mbatia
akifurahi jambo na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi CCM,Ndg. Nape
Nnauye.Katikati ni Katibu Mkuu wa CHADEMA,Dkt. Wilbroad Slaa.Picha na
Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
No comments:
Post a Comment