NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE MGENI RASMI MAADHIMISHO YA TAIFA LA IRAN
Balozi
wa Iran nchini Tanzania,Mh.Mehdi Aghajafari akimpokea Naibu Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh.Dkt.Mahadhi Juma Maalim (Mb)
alipowasili katika hafla ya kusherehekea siku ya Taifa la Iran
iliyofanyika kwenye makazi ya Balozi huyo Jijini Dar es Salaam jana
usiku.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mh.Dkt.Mahadhi
Juma Maalim (Mb) akizungumza mbele ya wageni mbalimbali walioalikwa
katika hafla ya siku ya Taifa la Iran iliyofanyika kwenye makazi ya
balozi wa Iran Jijini Dar es Salaam.
Balozi
wa Syria nchini, Mhe.Abdulmonem Annan (kushoto) Jaji mkuu wa Tanzania,
Mhe. Mohamed Chande Othman (katikati) na Balozi wa Yemen nchini,
Mhe.Abdulla Hassan Alamri wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi kwenye
hafla ya Siku ya Iran, Naibu waziri Dkt. Mahadhi.
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan
Simba Yahaya (kulia) akiwa na Maafisa kutoka Wizara hiyo Bw. Mkumbwa Ally (kushoto) na Bw. Leonce Bilauri (katikati) wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri (hayupo pichani) katika hafla hiyo.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe.Dkt.Mahadhi
Juma Maalim (Mb.) akisalimiana na Balozi wa Syria nchini Mhe. Abdulmonem
Annan kwenye sherehe hizo.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.Mohamed Chande Othman akizungumza jambo na Mhe.Dkt.Mahadhi kwenye hafla ya siku ya Iran.
Picha na Reuben Mchome
No comments:
Post a Comment