Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Bloggers Tanzania (TBN), Joachim Mushi
(kulia) akikabidhi ubani wa fedha shilingi 900,000 na kutoa pole kwa
mwanamziki mkongwe, John Kitime (kushoto) ambaye amefiwa juzi na mkewe,
tukio hilo lilifanyika jana Kimara eneo la Nguzo ya 800, jijini Dar es
Salaam. Mzee Kitime ni mwanachama wa TBN.
Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Bloggers Tanzania (TBN), Joachim Mushi
(kulia) akitoa ujumbe wa pole kwa John Kitime na waombelezaji mara baada
ya kukabidhi ubani wa fedha zilizotolewa na wanachama wa TBN jana eneo
la Kimara Nguzo ya 800 jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wajumbe wa TBN
walifika kumfariji Kitime ambaye pia ni mwanachama wa TBN
Baadhi ya wajumbe wa TBN, wakiwa katika picha na mzee Kitime walipofika
kumfariji na kutoa ubani wa TBN. Kutoka kushoto ni Sufian na Othman
Michuzi pamoja na Mzee Kitime.
Kutoka kushoto ni mjumbe mshauri na Kiongozi wa TBN, Issa Michuzi,
baadhi ya wanamuziki wa bandi ya Njenje, Mwenyekiti wa TBN, Mzee Kitime
na mwanae akipata picha na baadhi ya waombolezaji marafii waliofika
kumfariji.
Baadhi ya wanamuziki wa Njenje pamoja na wajumbe wa Chama cha Bloggers
Tanzania (TBN) wakipata picha ya pamoja na mfiwa mwanamziki mkongwe,
John Kitime walipofika msibani kumfariji jana Kimara eneo la Nguzo ya
800, jijini Dar es Salaam. Mzee Kitime ni mwanachama wa TBN.
Tanzania Bloggers Network Wamfariji Mzee Kitime kwa Kufiwa
Reviewed by
crispaseve
on
7:34 AM
Rating:
5
No comments:
Post a Comment