PICHA MAALUM KUTOKA IKULU:RAIS JAKAYA KIKWETE AFUNGUA JENGO LA KITEGA UCHUMI LA NSSF MOSHI
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt.Ramadhan Dau
pamoja na wadau wengine wakitazama ramani ya jengo jipya la kitega
uchumi la NSSF mjini Moshi Kilimanjaro Commercial Complex wakati wa
hafla ya ufunguzi.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua jengo la upasuaji katika hospitali
ya rufaa ya Mawenzi mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro muda mfupi baada ya
kulifungua Jana.Kulia ni Naibu Waziri wa Afya Dkt.Steven Kebwe.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
wauguzi wa hospitali ya rufaa ya
Mawenzi mjini Moshi muda mfupi baada ya
kufungua jengo la upasuaji na kuweka jiwe la msingi kuzindua ujenzi wa
wodi ya mama na watoto katika hospitali hiyo jana.(wanne kulia ni Naibu
waziri wa Afya Dkt.Steven Kebwe,wanne kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro Leonidas Gama,Kushoto ni Mbunge wa Vunjo Agustino Lyatonga
Mrema,na wapili kushoto ni Mbunge wa Moshi Vijijini Dkt.Cyril Chami.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na chipikizi wa
Tanzania Girl Guides wakati wa hafla ya ufunguzi wa jengo la kitega
uchumi la NSSF mjini Moshi jana.Tanzania Girl Guides,UMATI,Tanzania Red
Cross ni wadau wa NSSF katika mradi huo.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na mkurugenzi Mkuu wa NSSF
Dkt.Ramadhani Dau baada ya hafla ya ufunguzi wa jengo jipya la kitega
uchumi la NSSF mjini Moshi jana .Katikati ni Waziri wa Kazi na Ajira
Mh.Gaudensia Kabaka. Picha na Freddy Maro-IKULU
No comments:
Post a Comment