PICHA KUTOKA WIZARA YA MAMBO YA NDANI:WAZIRI CHIKAWE AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA KUPAMBANA NA VURUGU NA UGAIDI, WASHINGTON MAREKANI
Rais wa Marekani, Barack Obama akitoa hotuba yake katika Mkutano wa
Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani uliofanyika katika
Ukumbi wa Loy Henderson, Wizara ya Mambo ya Nje, jijini Washington DC
nchini humo leo. Mkutano huo uliowashirikisha Mawaziri wanaoshughulika
na masuala ya usalama kutoka mataifa mbalimbali duniani, Maafisa Waandamizi
wa Umoja wa Mataifa (UN), Vyama vya Kiraia na Sekta Binafsi ulijadili
masuala mbalimbali ya jinsi ya kupambana na
ugaidi pamoja na vurugu
mbalimbali dunaini. Katika hotuba yake, Obama alisema mapambano dhidi
ya watu wenye msimamo mkali hayawezi kulinganishwa na mapambano dhidi
ya waislamu. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe aliiwakilisha
Tanzania katika mkutano huo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akimsikiliza kwa
makini Rais Barack Obama (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba
yake katika Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani
uliofanyika katika Ukumbi wa Loy Henderson wa Wizara ya Mambo ya Nje,
jijini Washington DC nchini humo leo. Mkutano huo uliowashirikisha Mawaziri
wanaoshughulika na masuala ya usalama kutoka mataifa mbalimbali duniani,
Maafisa Waandamizi wa Umoja wa Mataifa (UN), Vyama vya Kiraia na Sekta
Binafsi ulijadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupambana na vurugu
na ugaidi dunaini. Katika hotuba yake, Obama alisema mapambano
dhidi ya watu wenye msimamo mkali hayawezi kulinganishwa na mapambano
dhidi ya waislamu, hivyo hakuna dini yoyote inayowajibika kwa ugaidi,
isipokuwa watu ndio wanaowajibika kwa vurugu na ugaidi.
No comments:
Post a Comment