Header Ads

MBUNGE JOSHUA NASSAR AWAONGOZA WANANCHI KATIKA MAKABIDHIANO YA HEKARI 92 ZA SHAMBA LA MADIIRA ARUMERU.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru,Dastan Malya akiwa na watendaji wengine wa serikali katika ofisi ya mtendaji wa kata ya Siela Sing’isi wakati mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar alipofika kwa ajili ya kwenda kutembelea Shamba la Madiira.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassar akitia saini katika kitabu cha wageni katika ofisi ya kata ya Siela Sing'isi alipotembelea katika kijiji hicho cha Sing'isi.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassar akiongozana na Diwani wa kata ya Mbunguni Paul Laizer maarufu kama Askofu (shoto) wakati alipowaongoza wakazi wa vijiji vya Sing'isi na Malala kwenda kuangalia shamba la Madiira ambalo hekari 92 zimetolewa kwa vijiji hivyo.
Wananchi wa vijiji vya Sing'isi na Malala wakitizama sehemu ya eneo la Shamba la Madiira lililotolewa kwa wananchi wa vijiji hivyo.

No comments:

Powered by Blogger.