Magazeti yanayomilikiwa na makampuni binafsi yaongoza nchini.

Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) alipokuwa akiongea na
waandishi wa habari Ikilu jana jijini Dar es salaam akiwa na mgeni wake Rais wa
Ujerumani Rais wa Ujerumani Joachim Gauck (kushoto). Rais Gauck yupo nchini kwa
ziara ya kikazi kwa siku tano. (Picha na
Benedict Liwenga-MAELEZO)
Na Eleuteri Mangi-
MAELEZO
Tanzania ni miongoni
mwa nchi zinazosimamia uhuru habari na inaongoza kwa kuwa wa vyombo vingi
habari yakiwemo magazeti.
Kauli hiyo ilitolewa jana
jijini Dar es salaam na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya
Kikwete alipokuwa akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kujua sababu
za kusimamisha uingizaji nchini gazeti la “The East African”, wakati wa mkutano
wa waandishi wa habari yeye na Rais wa Ujerumani Joachim Gauck.
Rais Kikwete alisema
kuwa gazeti hilo halikufuata utaratibu wa kusambazwa nchini kulingana na sheria
na taratibu za nchi, hata hivyo Serikali imeshawasiliana na wahusika na wameelekezwa
utaratibu wa kufuata kulingana na sheria za nchi.
“Tanzania injali na
kusimamia uhuru wa habari, kuna magazeti mengi yakiwemo ya kila siku, wiki ambayo
yanayomilikiwa na makampuni binafsi ikilinganishwa na magazeti yanayomilikiwa
na Serikali” alisema Rais Kikwete.
Rais kikwete aliyataja
magazeti yanayomilikiwa na Serikali kuwa ni pamoja na Daily News na Habari Leo
ikilinganishwa na magazeti yanayomilikiwa na makampuni binafsi ambapo aliyataja
magazeti hayo kuwa ni The Guardian, The Citizen, Majira, Mwananchi, Nipashe na
mengine mengi.
Rais wa Ujerumani na
msafara wake wapo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tano ambayo ni mwaliko
walioupata kutoka kwa Dkt. Kikwete alipotembelea Ujerumani hivi karibuni na
kutunukiwa tuzo ya kufanya vizuri katika suala la chanjo kwa watoto.
Ugeni huo wa Rais Gauck
watapata fursa ya kujionea maeneo mengi yenye vivutio vya watalii nchini
yakiwemo Visiwa vya Zanzibar na Arusha ambayo yanajulikana kwa utajiri wa
vivutio hivyo barani Afrika na duniani.
Ujio wa Rais Gauck nchini
na msafara wake unafuatia mahusiano mazuri yaliyopo kati ya nchi hizo mbili wa
muda mrefu kwa manufaa ya maendeleo ya wananchi wao kiuchumi, kisiasa na
kijamii.
No comments:
Post a Comment