Header Ads

Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Tanzania inawaagiza Wamiliki wote wa kumbi za filamu Tanzania Bara kutofanya maonesho ya hadhara ya filamu yenye jina la FIFTY SHADES OF GREY inayoongozwa na Sam Taylor Johnson na kutengenezwa na Michael De Luka, Dana Brunetti na E.L. James.

 Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo 
--- 

Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Tanzania inawaagiza Wamiliki wote wa kumbi za filamu Tanzania Bara kutofanya maonesho ya hadhara ya filamu yenye jina la FIFTY SHADES OF GREY inayoongozwa na Sam Taylor Johnson na kutengenezwa na Michael De Luka, Dana Brunetti na E.L. James.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Tanzania kukagua filamu hiyo yenye urefu wa saa 2:05 na kugundua kwamba haizingatii sheria na kanuni zinazosimamia tasnia ya filamu nchini. Maamuzi haya yamefanywa kulingana na ukiukwaji wa Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Na. 4 ya mwaka 1976 kifungu cha 15 (i) na kifungu 18(i na ii) ambayo ufafanuzi wa utekelezaji wake uko katika Kanununi za Sheria hiyo Kifungu cha 24 vifungu vidogo vya a,b,d,e,n na t

No comments:

Powered by Blogger.