AMIN SALMINI AAHIDI KUIBORESHA OFISI YA SERIKALI YA MTAA KATA YA TABATA, WAKIFANYA SHEREHE YA KUWASHUKURU WAPIGA KURA WAO.

Mtoto
wa Rais Mstaafu wa awamu ya tano Zanzibar, Amin Salmin, akimkabidhi Cheti,
Mwenyekiti wa UWT ambaye pia ni Kaimu Katibu wa CCM wa Tabata Relini, Shahani
Mtwawa, wakati wa Sherehe maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwashukuru Wapiga
Kura wa CCM, waliofanikisha kuchaguliwa kwa Viongozi wa Serikali ya Mtaa huo wa
Kata ya Tabata. Sherehe hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika Ofisi za
Serikali ya Mtaa Kata ya Tabata, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake mgeni
rasmi huyo, aliahidi kuiboresha Ofisi hiyo ya Serikali ya Mtaa wa Tabata kwa
kununua Fenicha za ofisi zisizopungua gharama ya Sh. M 1.5. Picha na
Sufianimafoto.com

Mtoto wa
Rais Mstaafu wa awamu ya tano Zanzibar, Amin Salmin, akisaini katika kitabu cha
wageni, mara tu baada ya kuwasili kwenye ofisi hizo.

Mtoto
wa Rais Mstaafu wa awamu ya tano Zanzibar, Amin Salmin, akimkabidhi Vifaa vya
michezo (Jezi na Mpira) Katibu Mwenezi
wa Kata ya Tabata Relini, Ramadhan Mazongera, wakati wa Sherehe maalum iliyoandaliwa kwa
ajili ya kuwashukuru Wapiga Kura wa CCM, waliofanikisha kuchaguliwa kwa
Viongozi wa Serikali ya Mtaa huo wa Kata ya Tabata. Sherehe hiyo ilifanyika
mwishoni mwa wiki katika Ofisi za Serikali ya Mtaa Kata ya Tabata, jijini Dar
es Salaam.

Mtoto
wa Rais Mstaafu wa awamu ya tano Zanzibar, Amin Salmin, akimkabidhi Vifaa vya
Michezo (Jezi na Mpira) Mwakilishi wa Tawi la CCM la Mti Mgandisho Tabata,
Bakari Mpakala, wakati wa Sherehe maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwashukuru
Wapiga Kura wa CCM, waliofanikisha kuchaguliwa kwa Viongozi wa Serikali ya Mtaa
huo wa Kata ya Tabata. Sherehe hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika Ofisi
za Serikali ya Mtaa Kata ya Tabata, jijini Dar es Salaam.

Sehemu
ya Kinamama waliojitokeza kwenye sherehe hiyo.
No comments:
Post a Comment