Header Ads

MAKALA YA SHERIA: JIHADHARI, HAUTARURUHUSIWA KUFANYA TRANSFER AU KUPATA HATI IKIWA UNA MKATABA WA SERIKALI ZA MITAA.


Hapo awali niliandika namna sheria isivyowaruhusu viongozi wa serikali za mitaa kuandaaa na kusimamia mauzo na manunuzi ya nyumba au viwanja. Nikasema kitu hicho hakiruhusiwi katika sheria na wanaofanya hivyo hakika wako katika makosa makubwa. Nikasisitiza kuwa wewe ambaye mkataba wako umeandikiwa serikali za mitaa ujue wazi kuwa mkataba wako wa manunuzi hauna hadhi kisheria. Huu ni ukweli ambao nitazidi kuusema ili kuwaepusha watu na usumbufu na ili watu wasiendelee kuingia katika utapeli huu. Ndio, huu ni utapeli na ni jinai. Ni sababu hizihizi zinazowaingiza watu wasio na hatia kwenye migogoro ya ardhi na kuwapotezea hela zao.

1.HUWEZI KUFANYA TRANSFER UKIWA NA MKATABA WA SERIKALI ZA MITAA.

Kwa wale ambao waliwahi kufanyia mikataba yao ya manunuzi ya nyumba/viwanja serikali za mitaa halafu wakaamua kwenda ardhi kubadili jina watakuwa wamekutana na hiki kitu ninachoongelea hapa. Ikiwa ulifanya manunuzi ya ardhi na ukasimamiwa na serikali za mitaa basi ujue huwezi kubadilisha jina kutoka kwa aliyekuuzia kuingia jina lako. Na hapo ni vyote yaani hati au leseni ya makazi. Huwezi kabisa kubadilsha kimojawapo kati ya hivyo ikiwa mkataba wako ni wa serikali za mitaa.

Kusoma zaidi BOFYA HAPA

No comments:

Powered by Blogger.