Header Ads

ZIARA YA MKURUGENZI MKUU WA NHC GEITA NA KAGERA YAHAMASISHA MAENDELEO

Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akiongea na kikundi cha vijana cha Mshikamano Wilayani Muleba alipokitembelea kuona namna kinavtumia mashine zilizotolewa na NHC ili kuongeza ajira kwa vijana. Bw. Mchechu amezitaka Halmashauri za Wilaya nchini kuunga mkono juhudi za NHC kwa kuwapatia vijana maeneo ya kufanyia kazi zao.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu ukiwa eneo la Mtukula linapojengwa jingo la kisasa la biashara na NHC ili kuvutia na kuchochea ukuaji wa biashara katika eneo hilo la mpaka wa Tanzania na Uganda. Eneo hili ndipo zilipokuwa nyumba ndogondogo zilizojengwa na NHC na baadaye kuharibiwa na mabomu ya Nduli Iddi Amin alipovamia nchi yetu mwaka 1978. NHC iliiomba  Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi kulirejeshea eneo hilo ili kujenga jengo hilo la kibiashara.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akikagua viwanja vya NHC Wilayani Chato vinavyokusudiwa kujengwa nyumba za gharama nafuu ikiwa ni program ya NHC ya kuzifikia Wilaya zote nchini.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu ukikagua nyumba za makazi za NHC Wilayani Chato alipotembelea Wilaya hiyo jana

No comments:

Powered by Blogger.