WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO AFANYA ZIARA KATIKA MKOA WA SIMIYU KUKAGUA MIRADI YA UMEME NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo
katika mkutano wake na wananchi wa kijiji cha Bushigwamala wilayani
Busega (hawapo pichani).
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akipokelewa na baadhi ya
watendaji kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Kanda ya Ziwa na
Nishati na Madini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa
Mwanza. Profesa Muhongo anafanya ziara katika mikoa ya Simiyu, Tabora
na Shinyanga lengo likiwa ni kukagua miradi ya umeme vijijini
inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na
Taneesco.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akisaini kitabu cha
wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega kabla ya kuanza ziara
katika wilaya hiyo ili kujionea utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini
pamoja na kuzungumza na wananchi.
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo kwenye
mkutano na wananchi wa kata ya Ijitu iliyopo wilayani Busega.
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akitoa maelekezo
kwa Meneja wa Tanesco- Kanda ya Ziwa Mhandisi Joyce Ngahyoma ( wa mwisho
kushoto) ya kuitaka Tanesco kuongeza kasi ya usambazaji wa umeme
vijijini.
Mkazi
wa kijiji cha Ihale kilichopo wilayani Busega mkoani Simiyu ambaye
jina lake halikupatikana mara moja akiuliza maswali mbele ya Waziri wa
Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na wananchi (hawapo
pichani) mara Waziri alipofanya mazungumzo na wananchi wa kijiji hicho
ili kusikiliza kero zao.
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akitoa maelekezo
kwa mtaalamu kutoka kampuni ya Symbion iliyopewa kazi ya kujenga
miundombinu ya umeme katika kijiji cha Nyamikoma kilichopo wilayani
Busega Bw. Steve Thomson (kushoto).
Meneja
wa Tanesco- Kanda ya Ziwa Mhandisi Joyce Ngahyoma, akifafanua jambo
mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na
wananchi wa kijiji cha Nyamikoma wilayani Busega (hawapo pichani).
No comments:
Post a Comment