Mbinu mpya za kusafirisha dawa za kulevya

. Baadhi ya wanawake wa Kitanzania waliofungwa
katika magereza ya China na Hong Kong, walishika ujauzito kama moja ya
mbinu ya kupitisha dawa za kulevya bila kugundulika kwenye viwanja vya
ndege na mipaka mingine ya kimataifa. Mwananchi limebaini.
Watanzania wanne walio katika magereza ya China na
Hong Kong walijifungua watoto kwa nyakati tofauti wakiwa wanatumikia
vifungo na wamekiri kuwa walibeba ujauzito kama mbinu ya kupitisha dawa
hizo bila kukaguliwa.
Watoto wanaozaliwa magereza baada ya kufikisha
mwaka mmoja hupelekwa katika vituo vya watoto yatima na kusomeshwa na
Serikali ya China hadi pale wazazi wao watakapomaliza adhabu.
No comments:
Post a Comment