WATANO WAJERUHIWA KWA RISASI KATIKA SHOO YA CHRIS BROWN HUKO MAREKANI

Watu watano wameripotiwa kupigwa risasi na kujeruhiwa mapema asubuhi ya leo(Jan.11) katika klabu ya usiku ya Fiesta iliyopo San Jose, California nchini Marekani.
Tukio hilo lilitokea wakati mwanamuziki Chris Brown
aki-perform jukwaani kibao chake cha Loyal katika party iliyopewa jina
la Capricorn Bash ambayo ilikuwa mahsusi kwa ajili ya kuwapongeza watu
waliozaliwa kati ya mwezi Dec.22 na Jan.19 ambapo staa huyo alikuwa mshereheshaji wa shughuli hiyo.
Mtandao wa San Jose Mercury umeripoti kwamba tukio hilo
lilitokea majira ya 1:20 usiku kwenye barabara ya Monterey Kabla ya
polisi wa doria kufika eneo la tukio na kukuta watu 4 wakiwa
wamejeruhiwa vibaya, wakati wengine watano wakikimbizwa hospitali
jirani.
Chris Brown amewajulisha mashabiki wake kuwa yupo salama
salimini baada ya kuandika ujumbe mfupi kwenye ukurasa wake wa Twitter
leo. ”I’m”, aliandika Brown.
Polisi wamewaweka kizuizini watu kadhaa waliohusika kwenye
shambulio hilo huku hali za majeruhi zikitajwa kuendelea vizuri. Tazama
tukio lilivyotokea hapo chini
No comments:
Post a Comment