Header Ads

Utiwaji saini mkataba wa kujenga tena umoja na kukiunganisha upya Chama Tawala cha Sudan Kusini cha Sudan People’s Liberation Movement (SPLM)

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza utiaji wa saini. Kutoka kulia ni  Mhe. Salva Kiir Mayardit  Rais wa Sudan Kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa SPLM na anayeongoza kundi linalojulikana kama SPLM in Government (SPLM-IG), Mhe Dkt. Riek Machar ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa SPLM na pia aliyekuwa Makamu wa Rais wa Sudan Kusini anayeongoza kundi la SPLM in Opposition (SPLM-IO) na Dkt. Deng Alor Kuol ambaye anaongoza kundi la SPLM Leaders- Former Detainees (SPLM Leaders – FD).
Nyuma yao ni mjane wa marehemu John Garang aliyekuwa Mwenyekiti wa SPLM Mama Rebecca Nyandeng de Mabior na Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. Thobias Makoba. Meza kuu toka kushoto  wakishuhudia utiaji saini huo ni Makamu wwa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Naibu Rais wa Afrika Kusini Mhe Cyril Ramaphosa.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto), Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) na Bw. Deng Alor Kuol wakionesha hati baada ya kutia saini mkatana wa  makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pongezi kwa Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto), Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) na Bw. Deng Alor Kuol

baada ya kutia saini mkatana wa  makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia wakati  Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) wakipeana mikono na kubadilishana nyaraka baada ya kutia saini mkatana wa  makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.

No comments:

Powered by Blogger.