TANZIA : MSUMBIJI WATANGAZA MAOMBOLEZO YA SIKU TATU

Pichani ni Rais wa sasa wa Msumbiji Armando Guebuza
Serikali ya msumbiji imetangaza maombolezo ya siku tatu
kufuatia vifo vya watu 69 waliokufa baada ya kunywa pombe ya kienyeji
inayodaiwa kuwa na sumu ambayo ni nyongo ya mamba wakiwa katika msiba
nchini humo.
Katika maombolezo hayo serikali hiyo imeamuru bendera zote
nchini humo kupepea nusu mlingoti huku ikiahidi kuwapa tiba stahili
waathirika wa pombe hiyo na kuwasaka watu waliohusika katika kuweka sumu
kwenye pombe hiyo ingawa mmoja kati ya watu hao tayari amekufa.
Baadhi ya waathirika wa pombe hiyo iliyotengenezwa kwa mtama
na mahindi na kuchanganywa na kinachosadikiwa kuwa ni sumu ya nyongo ya
Mamba bado wamelazwa katika hospitali za nchi hiyo kwa ajili ya
uangalizi wa afya zao sambamba na ,tiba.
No comments:
Post a Comment