RAIS FRANNCOIS HOLLANDE WA UFARANSA AHUDHURIA MAZISHI YA WACHORA VIBONZO WA CHARLIE HEBDO

Rais Franncois Holland akitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yenye miili ya mapolisi waliouwawa katika shambulio
Mazishi ya wachora vibonzo saba wa jarida la Charlie Hebdo
waliouwawa wiki iliyopita, yamefanyika mjini Paris Ufaransa huku watu
wengine waliouwawa katika duka nchini humo wakitajwa kuzikwa mjini
Yerusalem.
Aidha katika mazishi ya polisi waliouwawa katika mashambulizi
hayo yamefanyika maziko ya heshima ambayo pia yamehudhuriwa na Rais
Franncois Hollande.
Wiki iliyopita Ufaransa iligubikwa na mshtuko na taharuki kwa
siku tatu wakati ndugu wawili waliposhambulia jarida la Charlie Hebdo
kutokana na hasira kwamba jarida hilo limekuwa likikejeli dini ya
kiislamu.

Rais
Franncois Holland wa Ufaransa akipigiwa saluti na maafisa polisi nchini
humo wakati alipohudhuriwa mazishi ya polisi waliouwawa katika
shambulio

Majeneza yenye miili ya waandishi habari wa jarida la Charlie Hebdo ambayo imetajwa kuzikwa mjini Yerusalem

Waombolezaji wakiwa na nyuso za huzuni
No comments:
Post a Comment