Header Ads

Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi ameitaka jamii ya wafugaji wa Kimasai kuunga mkono jitihada za waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa na Mwenyekiti wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi kuikomboa kielimu jamii hiyo kwa kuhakikisha watoto wa kike wanakwenda shule badala ya kuolewa mapema.

Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa akionyesha kifimbo alichopewa na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, kama ishara ya kutambua mchango wake katika sekta ya elimu kwa watoto wa kike wa jamii ya Kimasai mkoani Arusha jana. Kulia ni Mama Siti Mwinyi. Picha na Mussa Juma  
----
 Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi ameitaka jamii ya wafugaji wa Kimasai kuunga mkono jitihada za waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa na Mwenyekiti wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi kuikomboa kielimu jamii hiyo kwa kuhakikisha watoto wa kike wanakwenda shule badala ya kuolewa mapema.

Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 20 ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Masai iliyopo wilayani Monduli jana, Mwinyi alisema inasikitisha wakati kuna watu wamejitolewa kuisaidia jamii hiyo, lakini bado kuna wazazi hawataki watoto wao wa kike wasome.

No comments:

Powered by Blogger.