KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AANZA ZIARA YAKE LEO WILAYA YA WETE MKOA WA KASKAZINI PEMBA.
Katibu Mkuu wa CCM,ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba,Ndugu Kassim Mabrouk,mapema leo alipokuwa akiwasili mjini Wilayani Wete mkoa wa Kaskazini Pemba tayari kwa kuanza ziara ya siku tano mkoani humo.Ndugu Kinana akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wako Kisiwani Pemba kwa ziara ya Kuhimiza na Kukagua utekeleza wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2010.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinaa akisalimiana na baadhi ya
Wanachama
wa CCM Wilaya ya Wete,alipowasili katika ukumbi wa Jamhuri,ambapo Ndugu
Kinana alipokea taarifa ya kazi ya chama na Utekelezaji wa Ilani na pia
kuzungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya.
Baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wakiwa katika
ukumbi wa Jamhuri wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozungumza nao mambo mbalimbali ikiwemo Utekelezaji wa Ilani.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Baadhi ya
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM katika ukumbi wa
Jamhuri mjini Wete mkoa wa Kaskazini Pemba mapema leo,Kinana alizungumza nao mambo mbalimbali ikiwemo Utekelezaji wa Ilani.
Pichani kati ni Meneja Utawala wa shirika la Ununuzi wa Karafu
(ZSTC),Bwa.Issa
Hassani akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pichani
kulia alipokwenda kutembelea Ghala la Karafuu na kuona zoezi la ununuzi
wa Karafuu katika Bandari ya Wete,Kaskazini Pemba.
Katibu wa CCM,Ndugu Kinana akitoka kutembelea na kukagua bei ya karafuu katika ghala la Karufuu katika bandari ya Wete-Pemba.
Ghala la Karafuu kama lionekanavyo pichani
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameambatana na wanachama
wengine wa chama hicho,wakitoka kutembelea Kikundi cha Ushirika cha
ufugaji wa samaki na uhifadhi wa Mazingira katika Jimbo la Gando,wilaya
ya Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata maelezo mafupi kutoka
kwa Mshauri wa kikundi,Bwa.Mwinyjuma Hamad juu ya Kikundi cha Ushirika cha ufugaji wa samaki na uhifadhi wa
Mazingira chenye idadi ya washirika wapatao 22,katika Jimbo la Gando,wilaya ya Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Mshauri wa kikundi (Organization for Gando Fishing, Farm &
Enviromental
Conservation) Bwa.Mwinyjuma Hamad akitoa maelezo mafupi kwa Katibu Mkuu
wa CCM,Ndugu Kinana nama mabaki ya miti yanavyoweza kutengenezwa na
kutumika kama mkaa ikiwa kama ni sehemu ya kusaidia kutunza mazingira.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki utengenezaji wa
Maseredani
(Majiko ya Mkaa) yanayotengenezwa kwa kutumia udongo,Majiko jayo
yanatengenezwa na Vijana wajasiliamali wapatao 21 katika kijiji cha
Chanjaani,shehia ya Ukunjwi Jimbo la Gando,wilaya ya Wete mkoa wa
kaskazini Pemba,ambapo mmoja wao alieleza kuwa wamekuwa wakifaidika na
mradi huo kwa kiasi kikubwa,ikiwemo na kujiongezea kipato kwa kuuza kwa
wingi majiko hayo,alisema kuwa asilimia 70 ya majiko yanatengenezwa
Pemba,hivyo imepunguza uingizwaji wa majiko kutoka nje.
Pichani
shoto ni Afisa Uhusiano wa Shirika la Umeme Zanzibar,Bwan Fakhi Othman
Sharif akiwaongoza Katibu Mkuu wa CCM ndugu Kinana
na
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenda kupokea taarifa ya
usambazaji wa Umeme na kushiriki kazi za Usambazaji umeme (kusimamisha
nguzo za umeme),katika kijiji cha Chanjaani,jimbo la Tambwe,Wete mkoa wa
Kaskazini Pemba.Mradi huo una thamani ya shilingi milioni 84.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana katikati,Balozi Ali Karume kushoto
na
Dkt.Maua Daftari pichani kulia wakishiriki kufukia mabomba ya maji
katika mradi wa usambazaji Maji katika Jimbo la Mtambwe,Wete mkoa
Kaskazini Pemba.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akizungumza na wanachama wa
Tawi la Kigangani,jimbo la Ole,Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana
alipowahutubia leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo mjini Wete,mkoa wa Kaskazini Pemba.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana
akiwahutubia baadhi ya Wananchi waliofika katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo mjini
Wete,mkoa wa Kaskazini Pemba.
















No comments:
Post a Comment