Header Ads

BUNGE LAENDELEA NA VIKAO VYAKE MJINI DODOMA

1
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage akijibu moja ya maswali yaliyoelekezwa kwenye wizara yake katika kipindi cha maswali na majibu Januari 30,2015  Bungeni mjini Dodoma.
2
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akijibu swali  Bungeni mjini Dodoma.
3
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dkt. Pindi Chana akijibu maswali kutoka kwa wabunge  mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
4
 Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akitoa maelezo wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini Dodoma.
5
 Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi akitoa kauli ya Serikali kuhusu Mkakati wa Serikali wa Kutatua Changamoto za Soko la Sukari nchini,  Bungeni mjini Dodoma.
6
Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Susan Lyimo akichangia hoja ya Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC), Kamati ya Bajeti na Kamati Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC)  Bungeni mjini Dodoma.
7
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa (kushoto) akiteta jambo na Mbunge wa Kuteuliwa na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia,  Bungeni mjini Dodoma.
8
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Ester Bulaya akichangia hoja ya ya Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC), Kamati ya Bajeti na Kamati Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) jana Bungeni mjini Dodoma.
9
Mbunge wa Mkanyageni Mohamed Habibu Mnyaa akichangia hoja Bungeni mjini Dodoma wakati wa kuchangia hoja za Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC), Kamati ya Bajeti na Kamati Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC).
10
Baadhi ya wageni waliohudhuria kwenye ukumbi wa Bunge la Jamhuri bungeni mjini Dodoma.
Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO, Dodoma
Mmoja wa Chipukizi akiwa amebebwa baada ya kuzimia akifanya mazoezi ya gwaride Bendi ya Vijana wa CCM kutoka Zimbabwe ikiongoza mazoezi ya gwaride Mkurugenzi wa TOT John Komba akizungumza na bendi ya vijana wa CCM kutoka Zanzibar Posted by Richard Mwaikenda at Saturday, January 31, 2015 0 comments Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest Magazeti Leo Jumamosi Posted by Richard Mwaikenda at Saturday, January 31, 2015 0 comments Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest PAC YAISHAURI SERIKALI NAMNA YA KUINUSURU KAMPUNI YA TTCL Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto (kulia) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deo Filikunjombe wakiwa katika majukumu yao. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto (kulia) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deo Filikunjombe wakiwa katika majukumu yao. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akiwa katika majukumu. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akiwa katika majukumu. KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imetoa mapendekezo ya kuinusuru Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kutokana na hali mbaya ya kampuni hiyo kifedha kwa sasa ambapo inaendeshwa kwa hasara huku ikiwa na madeni makubwa. PAC imetoa mapendekezo hayo katika taarifa yao kwa bunge ya mwaka juu ya ukaguzi wa hesabu za Serikali kwa mashirika ya umma iliyotolewa Januari 28 mwaka 2015. Kwa mujibu wa taarifa ya PAC hali ya mapato na matumizi ya TTCL kwa mwaka 2012 ilipata hasara ya bilioni 20.883 huku kwa mwaka 2013 ikipata hasara ya bilioni 16.258. PAC ilisema majumuisho ya hasara ya TTCL kupata hasara kwa takribani kwa miaka 10, Kampuni sasa imekuwa na hasara ambayo kwa mwaka 2013 ilifikia bilioni 334.48, jambo ambalo limeiondolea mvuto wa kukopeshwa na taasisi za fedha hata zile zenye nia ya kuikopesha. "...Ukosefu wa fedha za kutosha kutekeleza miradi ya Kampuni umekuwa kikwazo kwa TTCL kukabiliana na ushindani wa kibiashara. Kwa kipindi kirefu ufanisi wa TTCL kiuwekezaji na kifedha umeendelea kudorora. Tangu TTCL ibinafsishwe mwaka 2001, hakuna uwekezaji mkubwa uliofanyika na mpango wa kutafuta mkopo kutoka mabenki ya ndani na nje ya nchi unakwamishwa na masharti ya kupata udhamini wa Serikali," ilieleza taarifa hiyo ya PAC. PAC iliongeza kuwa ukiacha madeni yaliopo pia TTCL inadaiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) jumla ya bilioni 25 hivyo kufanya jumla ya deni kufikia bilioni 101.6. Kamati hiyo ya bunge imesema kuna umuhimu wa Serikali kufanya maamuzi ya haraka ya kuikwamua TTCL ili iweze kuendelea kutoa huduma kwenye Sekta ya Mawasiliano ikizingatiwa kuwa ndiyo inayoendesha Mkongo wa Taifa wa mawasiliano. Katika mapendekezo ya PAC ili kuikwamua TTCL imeishauri Serikali kununua hisa asilimia 35 zinazomilikiwa na Bharti Airtel katika TTCL kwa gharama ndogo kwani Bharti Airtel haikutimiza kikamilifu masharti ya mkataba wa mauziano ya hisa hizo hapo awali kwani tangu inunue hisa hizo haijafanya uwekezaji katika Kampuni ya TTCL. "...TTCL isamehewe deni la Serikali Sh. 76.6 bilioni na deni la TCRA Sh. 25 bilioni ambayo jumla yake ni Sh. 101.6 bilioni na fedha hizo zipelekwe kuongeza mtaji ili Kampuni itoke kwenye kuwa na mtaji hasi wa Sh. 87.896 bilioni na kuwa na mtaji chanya wa sh. 13.704 bilioni. Likifanyika hili basi Kampuni hiyo itaweza kukopesheka. Serikali ikamilishe taratibu zake za kuimilikisha TTCL Mkongo wa Taifa ili izidi kuuendeleza kwa ufanisi na kuongeza mapato ya TTCL," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo. Hata hivyo PAC imeshauri kuwa kuna umuhimu wa kufanya marekebisho ya muundo wa Kampuni ya TTCL kwani kwa sasa ina idadi kubwa ya wafanyakazi (1549) isiyoweza kuwalipa. Aidha, ilibainisha kuwa kwa sasa zinahitajika bilioni 32 kwa ajili ya kugharamia urekebishaji wa muundo wa Kampuni ili uendane na mahitaji ya utoaji wa huduma mbalimbali. Mashirika mengine yenye hali mbaya kifedha na uendeshaji ni pamoja na Shirika la Ndege Tanzania, ATCL ambayo kwa sasa ina madeni makubwa huku ikiwa na ndege moja aina ya Dash 8–Q 300, Wafanyakazi 142 na Jengo la ATC House lililoko mtaa wa Ohio, Dar es Salaam. Posted by Richard Mwaikenda at Saturday, January 31, 2015 0 comments Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest wakulima wa pareto wasaidiwa mbegu na miche ya zaidi ya Sh Mil 400 na kiwanda cha Pareto (PCT Meneja wa kiwanda cha pareto mafinga (PCT) Martine Oweka mkulima akiwa shambani akiendelea kufanya kazi shambani.hili ni shamba lilopo mbeya wakulima wakiwa shambani wakiendelea kufanya kazi shambani huko mbeya. hii ndio pareto yenyewe ikiwa tayari kwa kuvunwa na Tumaini Msowoya,iringa KIWANDA cha Pareto (PCT), cha Mafinga wilayani Mufindi kimetumia zaidi ya shilingi milioni 400, kwa ajili ya kuwasaidia wakulima mbegu na miche ya zao hilo, ili kukuza na kuinua zao hilo. Kila msimu wa Kilimo, kiwanda hicho kimekuwa kikisambaza mbegu na miche ya Pareto kwa wakulima wa zao hilo katika mikoa yote ambayo zao hilo limekuwa likistawi ikiwemo Iringa, Mbeya, Njombe na Arusha. Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa kiwanda hicho Martine Oweka alisema kuwa lengo lao ni kuhakikisha zao la Pareto ambalo ni mkombozi kwa mkulima. Oweka amewataka wakulima wa mikoa hiyo kulima zao hilo kwa wingi ili waweze kuinua kipato chao na kuondokana na umaskini kutokana na kuwepo kwa uhakika wa soko la zao hilo, tofauti na miaka ya nyuma kufuatia uwepo wa kiwanda. Oweka alisema ili wakulima waondokane na umaskini, lazima wajikite katika mazao ya biashara likiwemo pareto, kutokana na zao hilo kwa sasa kuwa na bei nzuri katika soko la dunia. Alisema kuwa endapo wakulima wa mkoa wa Iringa na mingine inayostawisha zao hilo wataamua kulima pareto kama zao mama la biashara wanaweza kuondokana na umaskini, kutokana na ukweli kwamba, zoko la pareto limekuwa na uhakika tofauti na miaka ya nyuma wakati soko la zao hilo lilipoyumba. Aliongeza kuwa kwa sasa kiwanda chao kinalima zaidi ya ekari 300 za pareto, na kwamba kazi kubwa iliyopo ni kuhakikisha kuwa wakulima wanalima zao hilo na kufuatilia hatua zote za kupanda, kuvuna, kukausha na kusafirisha hadi kiwandani. Akizungumzia masoko ya kimataifa Oweka alisema kuwa kwa sasa zipo nchi nyingi ambazo zinauhitaji mkubwa wa zao la pareto na ndiyo maana bei yake ipo juu. Alizitaja nchi hizo kuwa ni Japani, India, Australia na nchi zilizopo bara la Ulaya kuwa wananunua pareto kwa wingi. Posted by Richard Mwaikenda at Saturday, January 31, 2015 0 comments Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest Rais Kikwete akiwa kwenye Mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa,Ethiopia Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipitia moja ya taarifa wakati akiwa kwenye Mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa,Ethiopia leo.Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika (kulia) wakikutana na marais wastaafu, Thabo Mbeki wa Afrika ya Kusini(Kushoto) na Joachim Chissano wa Msumbiji(wapili kushoto) wakati wa mkutano wa 24 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika unaofanyika Addis Ababa Ethiopia leo. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Malawi Professa Peter Mutharika jijini Addis Ababa Ethiopia leo.Viongozi hao wanahudhuria mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais wa Malawi Professa Peter Mutharika(Wanne kushoto), Rais mstaafu wa Msumbiji Joachim Chissano, Rais mstaafu wa Afrika ya Kusini Thabo Mbeki(kulia) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe (kushoto)wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya kukutana wakati wa mkutano wa wakuu wan chi wanachama wa AU unaofanyika jijini Addis Ababa Ethiopia(picha na Freddy Maro) Posted by Richard Mwaikenda at Saturday, January 31, 2015 0 comments Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest Older Posts Home Wanaotembelea Blogu hii Sparkline 2160332 MATOKEO YA KIDATO CHA PILI MATOKEO YA KIDATO CHA PILI BOFYA HAPA KUTAZAMA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE HAYA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2013 HAYA HAPA Tanzania National Flag Tanzania National Flag Time Dar es Salaam The Digital Company The Digital Company Mtayarishaji: Mtayarishaji: Richard Mwaikenda BONGO HITS Find more music like this on GongaMx Blog Archive

Copy and WIN : http://bit.ly/copynwin

No comments:

Powered by Blogger.