Balozi wa Tanzania nchini ujerumani Philip Sang'ka Marmo awasilisha Hati za Utambulisho kwa Papa Francis

Baba Mtakatifu Francis akimsalimia Mtoto wa Mmoja wa Maafisa walioambatana na Balozi Marmo

Balozi Marmo akiwa katika picha ya pamoja na Baba Mtakatifu Francis

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Mhe. Philip Sang'ka Marmo, amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francis, Vatican-Roma, Italia. Balozi Marmo anawakilisha Ujerumani
na ndiye anayemwakilisha Mheshimiwa Rais kwa Baba Mtakatifu (Holy See).
Kwa utaratibu Mabalozi waliopo Italia hawaruhusiwi kuwakilisha nchi zao
kwa Baba Mtakatifu yaani Holy See. Nchi
nyingine ambazo Mhe. Balozi Marmo anawakilisha ni Austria, Bulgaria,
Jamhuri ya Czech, Hungaria,Ujerumani, Poland, Slovakia, Romania na
Switzerland.
No comments:
Post a Comment