Header Ads

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi,Profesa Anna Tibajuka Akutana na Waandishi wa Habari Jijini Dar na Kutoa Msimamo Wake Kwamba Hana Sababu ya Kujiuzuru Kwenye Nafasi Yake Kwa Kuwa Hakuhusika Kwa Namna Yeyote Kwenye Sakata la Uchotwaji wa Mabilioni Kwenye Akaunti ya Escrow.


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi,Profesa Anna Tibajuka akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa mikutano kwenye hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es salaam leo.
 Sehemu ya Waandishi wa Habari waliofika kwenye Mkutano huo ulioitishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi,Profesa Anna Tibajuka.
Sehemu ya Umati wa Waandishi wa Habari.Picha na Chalila Kibuda-Globu ya Jamii
 na Video MichuziTV
----
Siku Moja baada ya kujiuzuri kwa Mwanasheria mkuu Jaji Fredrick Werema, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kwa mara nyingine amejitokeza hadharani na kutoa msimamo wake kwamba hana sababu ya kujiuzuru kwenye nafasi yake kwa kuwa hakuhusika kwa namna yeyote kwenye sakata la uchotwaji wa mabilioni kwenye akaunti ya Escrow.
Akizungumza na waandishi wa habari asubuhi jijini Dar es Salaam, Profesa Tibaijuka amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa shinikizo la kutaka kujiuzuru, yeye binafsi ameona hana sababu ya kufanya hivyo kwani kufanya hivyo ni kukubali kuwa amehusika moja kwa moja kwenye kashfa hiyo jambo ambalo si la kweli.

No comments:

Powered by Blogger.