SOMA TAARIFA YA UFAFANUZI NA KANUSHO KUTOKA WIZARA YA NISHATI NA MADINI KUHUSU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter
Muhongo (Mb)
--
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Utendaji
wa Wizara chini ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter
Muhongo (Mb)
Taarifa
za gazeti hilo zilieleza kuwa utendaji wa Wizara ya Nishati na Madini
hasa katika uongozi wa Waziri Muhongo umekuwa ni wa kukatisha tamaa.
Moja ya mifano iliyotolewa ni kuendelea kuwepo kwa wachimbaji madini
wanaozidi kutorosha madini kwa nia ya kukwepa kodi. Hoja hii haina
ukweli wowote kwani chini ya uongozi wa Waziri wa Nishati na Madini,
Prof. Sospeter Muhongo (Mb) utendaji wa Wizara umeimarika kwa kiasi
kikubwa. Chini ya Uongozi wake kumekuwepo na uwajibikaji mkubwa kwa
watumishi wa wizara ili kuhakikisha kuwa wanawatumikia wananchi
ipasavyo. Ni katika kipindi chake kumekuwepo na uanzishwaji wa
madawati ya ukaguzi wa madini katika viwanja vikubwa vya ndege vya
JNIA, KIA na Mwanza chini ya Wakala wa Ukaguzi wa madini (TMAA) ili
kudhiditi wachimbaji madini na watu wengine wenye nia ya kutorosha
madini nje ya nchi bila kuzingatia sheria.
Kutokana na hatua hiyo
madini mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 15
yameweza kukamatwa. Madini yaliyokatwa bila kuwa na vibali halali
yametaifishwa na Serikali. Serikali ilianza kuuza baadhi ya madini
yaliyokamatwa kwa njia ya mnada kwenye Maonyesho ya Vito
yaliyofanyika Mjini Arusha kuanzia tarehe 18 - 20 Novemba, 2014.
Katika mnada huo jumla ya zaidi ya shilingi milioni 70 zilipatikana
na kuingia Serikalini. Serikali itaendelea kupiga mnada madini
mengine yaliyokamatwa kwa manufaa ya taifa. Wizara inaendelea
kuimarisha udhibiti ili kuhakikisha kuwa mtu yeyote anayekusudia
kutorosha madini anakamatwa na kuchukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na
madini yake kutaifishwa na Serikali. Katika kusimamia sheria na
taratibu, chini ya Uongozi wa Prof.Muhongo, Wizara imedhibiti tabia
ya kuchukua vitalu vya madini na kuhodhi ili wale tu wanaozingatia
masharti ya leseni ndio waendelee kuvifanyia kazi vitalu. Hili
limewaumiza waliokuwa na tabia hiyo ambao kimsingi walikuwa wanavunja
sheria. Baadhi ya vitalu vilivyopokonywa vimekuwa vikigawiwa kwa
wachimbaji wadogo.
Hivyo, si kweli kwamba utendaji wa Wizara ya
Nishati na Madini chini ya Prof. Sospeter Muhongo (Mb) ni wa
kukatisha tamaa katika kudhibiti utoroshaji wa madini nje ya nchi na
katika ukiukwaji wa masharti ya leseni mbalimbali za madini kama
ilivyodaiwa.
Upitiaji
Mikataba ya Madini
Taarifa
za gazeti hilo la NIPASHE la Jumatatu tarehe 08 Desemba, 2014
zilieleza kuwa chini ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter
Muhongo (Mb) Serikali imeshindwa kupitia mikataba ya madini ili taifa
linufaike zaidi. Taarifa hizo si za kweli zinalenga kupotosha umma.
Ukweli
ni kuwa chini ya Uongozi wa Waziri wa Nishati na Madini, Prof.
Sospeter Muhongo (Mb), Wizara imepitia mikataba ya madini kwa kufanya
majadiliano na Kampuni za uchimbaji madini zenye mikataba ili
kurekebisha vipengele vya mikataba ambavyo vinalenga kuleta manufaa
zaidi kwa Taifa. Kazi hiyo imefanyika kwa Kampuni zote zenye mikataba
na tarehe 9 Oktoba, 2014 Kampuni ya Geita Gold Mine (GGM) imetiliana
saini mkataba wa kurekebisha vipengele katika mkataba uliosainiwa
huko nyuma baada ya majadiliano kukamilika.
Aidha, majadiliano na
Kampuni ya ACACIA (zamani Kampuni ya African Barrick Gold –ABG)
yamekamilika na kilichobaki ni pande mbili (Serikali na Kampuni)
kusaini marekebisho yaliyofanyika kwa ajili ya mikataba ya migodi
yake ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara.
- KUKATIKA KWA UMEME
Kukatika
kwa umeme kunasababishwa na kuzeeka kwa miundombinu ya usafirishaji
na usambazaji umeme. Ikumbukwe kuwa, kwa kipindi cha karibu miaka
kumi TANESCO iliwekwa chini ya PSRC kwa nia ya kubinafsishwa mwaka
1997 – 2007. Katika kipindi hiki TANESCO haikuruhusiwa kuwekeza
wala kufanya ukarabati wa miundombinu yake hivyo hali hiyo ilipelekea
kuchakaa kwa miundombinu hiyo ikiwemo mfumo wa usafirishaji na
usambazaji wa umeme. Hata hivyo baada ya Serikali kubadili mtazamo
wake wa kulibinafsisha Shirika, TANESCO mipango kabambe ya kufanya
ukarabati wa miundombinu hiyo na kujenga mipya ili kuwa na mfumo wa
usafirishaji na usambazaji umeme ulio wa uhakika. Kazi hiyo
inaendelea katika sehemu mbalimbali nchini ikiwemo jiji la Dar es
Salaam ambako kazi ya kukarabati na kupanua miundombinu ya usambazaji
umeme inaendelea.
Aidha, TANESCO ilishaelekezwa kutoa taarifa kwa
umma kuhusu katizo lolote la umeme lililopangwa kwa ajili ya
matengenezo ya miundombinu ya umeme. TANESCO imekuwa ikifanya hivyo
kwa kutumia vyombo vya habari vikiwemo televisheni, radio na magazeti
na pia kwa kutumia magari ya TANESCO kufikisha taarifa kwa maeneo
yanayoathirika. Kwa upande wa katizo la umeme usiotarajiwa, TANESCO
inacho kikosi cha dharura ambacho watumishi wake wanafanya kazi masaa
ishirini na nne kwa zamu ili kuhakikisha kuwa hitilafu ndogondogo
zinatatuliwa mara moja zinapojitokeza. Jamii ya Watanzania
wanalishuhudia hilo.
- DENI LA TANESCO LAPAA.
Mpaka
kufikia mwanzoni mwa mwaka 2014, deni la TANESCO lilikuwa limefikia
takribani Shilingi bilioni 695.30. TANESCO kwa kutumia vyanzo vyake
vya fedha kutokana na ukusunyaji wa maduhuli ndani ya kipindi cha
miezi 11 imepunguza deni hilo mpaka kufika takribani Shilingi bilioni
355.11. Kukua kwa deni la TANESCO kulisababishwa na hali ya ukame
uliolikumba taifa kuanzia miaka ya 2011 ambapo TANESCO ililazimika
kununua umeme aghali kutoka kwa wazalishaji wa umeme binafsi ikiwemo
mitambo ya kukodi ya dharura. Deni hilo lilikua kama ifuatavyo:
Mwaka
Deni (Bilioni Sh.)
2011
538.47
2012
563.02
2013
695.30
2014
(9
Disemba)
355,11
TANESCO
imeongeza ufanisi wake katika kukusanya maduhuri na kufikia kiwango
cha asilimia 97 na fedha inayopatikana inatumika kupanua huduma ya
umeme nchini, kuendesha Shirika na kulipa madeni inayodaiwa.
Ukweli
ni kwamba deni la TANESCO limeshuka kwa kiasi kikubwa na kwa sasa
TANESCO imeweka mkakati maalumu wa kuwalipa wadeni wake wakubwa kiasi
cha Shilingi bilioni tatu kwa wiki kwa kila mdai, hivyo ni matarajio
ya Shirika kumaliza deni hilo mwaka kesho (2015).
- NCHI ITASONGA MBELE
Wazo
la kuanzishwa kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) lilibuniwa na
watumishi na viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini mwaka 2005/6
chini ya uongozi wa Nazir Karamagi akiwa Waziri wa Nishati na Madini.
Taratibu za kuanzishwa kwa REA zilikamilika mwaka 2007 ambapo REA
ilianza kutekeleza majukumu yake.
Mheshimiwa
Sospeter Muhongo baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini
ameisaidia REA kupata fedha kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo
na hivyo amesaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza kwa kasi ya kupeleka
huduma ya umeme vijijini.
Aidha,
Ili kufikia lengo la kuwaunganishia umeme asilimia 30 ya watanzania
ifikapo mwaka 2015, Chini ya uongozi wa Waziri Muhongo Serikali
kupitia TANESCO, ilipunguza gharama za kuunganisha umeme wa njia moja
(single phase) kwa wateja wadogo kwa wastani wa kati ya asilimia 30
na 77 kama ifuatavyo:
Kwa wateja watakaojengewa njia moja (single phase) kwenye umbali usiozidi mita 30 bila kuhitaji nguzo, katika maeneo ya vijijini watalipa Shilingi 177,000 na wa mijini watalipa Shilingi 320,960 badala ya Shilingi 455,108 zinazolipwa na wateja hao kwa sasa.
Kwa wateja watakaojengewa njia moja (single phase) na kuwekewa nguzo moja, katika maeneo ya vijijini ni Shilingi 337,740 na wa mijini ni Shilingi 515,618 badala ya Shilingi 1,351,884 zinazolipwa na wateja hao kwa sasa.
Kwa wateja watakaojengewa njia moja na kuwekewa nguzo mbili katika maeneo ya vijijini ni Shilingi 454,654 na wa mijini ni Shilingi 696,670 badala ya Shilingi 2,001,422 zinazolipwa na wateja hao kwa sasa.
Kwa
ujumla katika kipindi hiki huduma ya umeme nchini imepanuka na kuwa
bora zaidi kuliko siku za nyuma. Ni matarajio ya Serikali kuwa huduma
hii itazidi kuwa bora zaidi katika siku chache zijazo kutokana na
juhudi kubwa zinazoendelea katika sekta ndogo ya umeme.
- DALALI WA FEDHA ZA ESCROW
Waziri
wa Nishati na Madini ndiye msimamizi mkuu wa masuala yanayohusu sekta
za Nishati na Madini nchini. Mtambo wa IPTL ulijengwa kwa ajili ya
kufua umeme unaotumiwa na jamii ya watanzania. Kuwepo kwa mgogoro
kungeweza kuondoa azma ya uwepo wa mtambo huo ya kufua umeme ili
kuliepusha Taifa kuingia katika mgawo wa umeme kutokana na upungufu
wa upatikanaji wa nishati hiyo, hivyo lilikuwa ni jukumu lake kuona
kuwa mgogoro wa wawekezaji wa mitambo ya IPTL unakwisha ili mitambo
iendelee kutoa huduma ya umeme kwa Taifa. Jukumu la Waziri ni
kusimamia Sera, Sheria na taratibu katika sekta anazozisimamia.
Katika kufanya hivyo, Waziri hukutana na wadau na kujadili masuala
kwa uwazi bila kificho kwa nia ya kujenga nchi na kuhakikisha kuwa
maslahi ya Taifa ndiyo kipaumbele. Kwa hiyo mikutano na Wadau ikiwa
ni pamoja na wawekezaji hufanyika si kwa udalali. Suala la fedha za
akaunti ya Escrow lilihusu uamuzi wa mahakama iliyojiridhisha kuwa
mnunuzi wa hisa zote za VIP na MECHMAR ni halali na alitakiwa
kukabidhiwa mali na madeni ya IPTL. Mali ni pamoja na kiasi cha fedha
stahiki kwenye Akaunti ya Escrow ambazo hata hivyo ilidhihirika kuwa
hazitoshi kukidhi deni halali.
Akaunti
hiyo ilikuwa na Sh. 182 bilioni wakati malipo yaliyokubalika kwa
pande zote (IPTL na TANESCO) kwa mujibu wa maamuzi ya ICSID I
yalikuwa Sh. 306 bilioni. Kumwita Waziri wa Nishati na Madini kuwa
ni dalali ni kupotosha ukweli.
No comments:
Post a Comment