SERIKALI YAKUBALI AZIMIO ARUSHA KUHUSU HIFADHI YA JAMII
Waziri
wa Fedha Saada Mkuya Salum akitoa hotuba ya kufunga kongamano la
Kimataifa la siku tatu kuhusu hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17,
2014 jijini Arusha.(Picha zote na Eleuteri Mangi- Arusha).
Na Mwandishi wetu, Arusha
SERIKALI
ya Tanzania imeridhia azimio la arusha kuhusi hifadhi ya jamii nchini
Tanzania na kusema litatumika kama dira katika kunemeesha watanzania.
Azimio hilo ambalo limetoka baada ya mkutano wa siku tatu wa wadau
mbalimbali wa hifadhi ya jamii kutoka bara la Afrika na mashirika ya
kimataifa limeelezwa kuwa msingi mkubwa wa ajenda ya Tanzania
kuhakikisha wananchi wake wanahaki sawa katika elimu, afya na mwendelezo
wa kiuchumi. Lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba hifadhi ya jamii
inasaidia kuwa na maendeleo endelevu kwa kuangalia maendeleo ya binadamu
katika ujumla wake.
Mkutano
huo wa siku 3 uliohusisha wataalamu 150 kutoka sekta mbalimbali nchini
na barani Afrika wakiwemo watengeneza sera, watafiti na wataalamu wa
masuala ya hifadhi. Ukiwa umewezeshwa na serikali ya Tanzania kwa
kushirikiana na UNICEF, ILO, UNAIDS na taasisi ya utafiti wa sera za
uchumi EPRI iliyopo Afrika Kusini (EPRI) , mkutano huo umeelezwa na
waziri wa fedha Saada Mkuya Salumkwamba umeweka misingi imara ya kuwa
na hifadhi ya jamii endelevu inayojibu mipango ya maendeleo ya taifa.
Katibu
Mkuu Wazara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile akisoma Azimio la Arusha
linalohusu hifadhi ya Jamii, alisema kuwa historia imejirudia ambapo
yapata miaka 47 (1967-2014) iliyopita Tanzania ilipitisha Azimio la
Arusha lililolenga kupambana na maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi
na umaskini ambao Baba wa Taifa Mwl. Julius Kmbarage Nyerere aliwaita ni
maadui wa taifa.
Kukiwa
na wataalamu waliobobea katika mifumo ya hifadhi ya jamii kutoka
Afghanistan, Bangladesh, Ethiopia, Ghana, Kenya, Lesotho, Malawi,
Msumbiji, Afrika Kusini, Uganda, Zambia na Zimbabwe ulifanikiwa
kutengeneza hoja zitakazotumika kufanya hifadhi ya jamii Tanzania kuwa
endelevu.
Waziri
Mkuya alishukuru kwa ushiriki wa mkutano na jinsi ulivyokuwa wazi na
jinsi wataalamu walivyoweza kutengeneza azimio ambalo linaenda kuwa
msingi katika utengenezaji wa sera na sheria kuhusu hifadhi za jamii
nchini Tanzania na afrika kwa ujumla.
Mada
kadhaa ziliwasilishwa katika mkutano huo ambazo zilizaa majadiliano
yenye manufaa kuhusu mwelekeo wa hifadhi za jamii,utengenezaji wa mifumo
ya kuweza kuendelea kuwepo kwa hifadhi ya jamii na umuhimu wa uratibu
ndani ya serikali kuu, mitaa na mashirika yanayiotoa huduma za hifadhi
ya jamii.
Mwakilishi
wa UNICEF Tanzania, Jama Gulaid (kushoto) na Naibu Waziri wa Mambo ya
ndani ya nchi, Mhe. Pereira Silima (Mb) wakisikiliza azimio la Arusha
linalohusu hifadhi ya jamii wakati wa kufunga kongamano hilo.
Waziri
huyo alisema kwamba wakati taifa linaelekea katika uchumi wa gesi
utakaofanya kuwa na kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 masuala ya
hifadhi ya jamii yatakahakikisha haki katika kugawa keki ya taifa na
kuhakikisha kwamba kila mwananchi anapata huduma za elimu, afya, na za
kiuchumi kwa haki, kwa kuwa mifumo hiyo pia itatakiw akuchochea ajira na
ujasirimali huku ilkilinda afya za wahusika.
Kwa
upande wake Mwakilishi wa UNICEF nchini Dkt. Jama Gulaid akitoa neno la
shukrani aliisifu Tanzania kwa kuanza mapema kusimamia masuala ya kinga
ya jamii ikiwemo mifuko ya hifadhi ya jamii na misaada inayotolewa na
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kupitia mpango wake wa kunusuru kaya
maskini zilizo katika mazingira hatarishi.
Aidha,
Dkt. Gulaid aliipongeza Tanzania kwa kuwa na wimbo wa taifa
unaozungumzia watu akiwataja kuwa ni wanawake, wanaume na watoto pamoja
na bara la Afrika na watu wake licha ya kuwa na vivutio vizuri vya mlima
Kilimanjaro, hifadhi ya Serengeti na visiwa vya karafuu.
Mwakilishi wa UNICEF nchini Dkt. Jama Gulaid akitoa neno la shukrani
wakati wa kufunga kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya
Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha na aliisifu na
kuipongeza Tanzania kwa kuwa na wimbo wa taifa unaozungumzia watu
akiwataja kuwa ni wanawake, wanaume na watoto pamoja na bara la Afrika
na watu wake.
“Wimbo
huu wa Tanzania tofauti na nyimbo za nchi nyingine ambazo wao
wanazungumzia askari, watumwa, watawala wakiwemo Malkia na
Wafalme”alisema Dkt. Gulaid. Dkt. Gulaid aliwahakikishia wajumbe wa
mkutano huo kuwa wote wapo salama na wapo kwenye mpango wa hifadhi ya
jamii kwa kuwa wametambuliwa na kubarikiwa na wimbo wa taifa wa Tanzania
ambapo wajumbe waliimba wimbo huo na kuhitimisha kongamano hilo.
Washiriki
wa Kongamano hilo wakiimba wimbo wa Taifa baada ya Mwakilishi wa UNICEF
nchini Dkt. Jama Gulaid kutoa ombi kabla ya kumalizika kwa kongamano
hilo.
No comments:
Post a Comment