Header Ads

RAIS WA ZANZIBAR DR ALI SHEIN ASHIRIKI MAZIKO YA MUASISI WA CCM


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi AlhajDk.Ali Mohamed Shein(wa tatu kulia) pamoja na Viongozi na Waislamu wakibeba Jeneza lenye mwili wa Muasisi wa CCM  Marehemu Mzee Juma Ameir Juma  baada ya kumswalia katika Msikiti wa Abdalla Rashid Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi  na kwenda kuzikwa Jana kijiji kwao Muungoni Wilaya ya Kusini Unguja.
  Waombolezaji wakilibeba jeneza lenye mwili wa marehemu muasisi wa CCM marehemu Mzee Juma Ameir Juma aliyefariki jana na kuzikwa  kijijini kwao Muungoni  Mkoa wa Kusini Unguja,ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein  aliongoza maziko hayo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhaj Balozi Seif Ali Iddi (katikati) pamoja na Waislamu na Wananchi mbali mbali wakishiriki katika Maziko ya  muasisi wa CCM  Marehemu Mzee Juma Ameir  Juma aliyefariki usiku wa kuamkia jana na kuzikwa  kijijini kwao Muungoni wilaya ya Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akitia udongo katika kaburi la muasisi wa CCM  Marehemu Mzee Juma Ameir  Juma aliyefariki usiku wa kuamkia jana na kuzikwa  kijijini kwao Muungoni wilaya ya Kusini Unguja.Picha IKULU-Zanzibar

No comments:

Powered by Blogger.