Header Ads

Mwenyekiti mweza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Dk Emmanuel Makaidi amejitolea kusuluhisha mgogoro baina ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na chama chake cha Chadema.


 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na  Mbunge wa Kigoma Kaskazini -Chadema Zitto Kabwe walipokua wakiondoka katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam  baada ya kuwasilisha maoni ya chama hicho juu ya uundwaji wa Katiba Mpya, kwa viongozi wa tume ya kukusanya maoni hayo,Mapema Mwaka Huu. Picha Salhim Shao
Mwenyekiti mweza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Dk Emmanuel Makaidi 
-----
  Mwenyekiti mweza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Dk Emmanuel Makaidi amejitolea kusuluhisha mgogoro baina ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na chama chake cha Chadema.
 
Hatua ya mwanasiasa hiyo mkongwe ambaye pia ni Mwenyekiti wa NLD, imekuja siku chache baada ya kuibuka hoja mbalimbali katika mitandao ya kijamii zikishawishi Zitto kurejea Chadema hasa baada ya kauli yake bungeni kuwa amekuwa akiwakosa wanasiasa wenzake wa upinzani wanaounda kundi la Ukawa.
Ijumaa wiki iliyopita, Zitto alikaririwa na gazeti hili akisema yuko tayari kurudi Chadema kwa sharti kwamba mgororo baina yao ujadiliwe kwa uwazi na upande wenye makosa uombe radhi kwa uwazi pia, huku Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akisema suala hilo lina njia zake na siyo la kuzungumza katika vyombo vya habari.

No comments:

Powered by Blogger.