Mwanahabari Kibiki atangaza kuwania Ubunge jimbo la Iringa mjini
huyu ndiye mjumbe wa Mkutano Mkuu wa
CCM Taifa Frank Kibiki aliyetangaza nia.
Na fredy mgunda,iringa.
MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa
CCM Taifa, Frank Kibiki, ametangaza nia ya kuwania ubunge
wa jimbo la
Iringa mjini, kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza na waandishi wa
Habari leo ofisini kwake, Kibiki amesema ni
wakati wa vijana kushika hatamu kwa kuwania nafasi mbali mbali, ndani ya
CCM na
hatimaye kwenye umma wa watanzania.
Kibiki ambaye ni Katibu
mwandamizi wa Umoja wa Vijana, katika
wilaya mbali mbali nchini amesema ameamua kuomba kupitishwa nafasi hiyo
na CCM
ili aweze kusaidiana na wananchi wa manipaa ya Iringa katika kuwaletea
maendeleo.
Mjumbe huyo wa Mkutano mkuu
wa ccm Taifa, amedai kuwa zipo changamoto
nyingi zinazowakabili vijana na wananchi kwa ujumla na kwamba, njia
pekee ya
kuzitatua ni kuwa na uwakilishi toka miongoni mwao kwenye vyombo vya
maamuzi.
Kitaaluma, Kibiki ni
mwandishi wa habari mwandamizi kupitia
magazeti ya Uhuru na Mzalendo, mkoani Iringa.
No comments:
Post a Comment