Mtandao wa Wanawake na Katiba wataja sababu za kuvutiwa na Katiba pendekezwa
MTANDAO
Wanawake na Katiba nchini pamoja na Chama cha Wanahabari Wanawake
(TAMWA) wamesema wanaunga mkono Katiba iliyopendekezwa na kujivunia
hatua waliopiga katika kudai haki mbalimbali za mwanamke kwenye Katiba
hiyo ukilinganisha na ile ya Mwaka 1977.
Mtandao huo umetoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na
wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kuzungumzia hatua ambayo
mtandao huo unaoshirikisha zaidi ya hasasi 50 zinazopigania haki anuai
katika jamii.
Akizungumza
katika mkutano huo na wahariri wa habari, Mjumbe wa Mtandao huo, Dk.
Ave Maria Semakafu alisema harakati za kutetea haki za binadamu na
hususani za wanawake na watoto zilipata mwanya katika mchakato wa Katiba
uliyomalizika jambo ambalo alisema ni hatua kubwa ya safari ya
kumkomboa mwanamke.
Dk.
Maria Semakafu alisema kwa kuona mwanya nahatua waliopiga wanaharakati
katika masuala hayo, kwa kupitia Mtandao wa Wanawake na Katiba pamoja na
TAMWA wanaiunga mkono Katiba Pendekezwa kwa kile kuwa na utofauti
mkubwa kimaboresho ukilinganisha na ile ya mwaka 2014. Alibainisha kuwa
licha ya mapungufu kidogo yaliopo lakini umoja huo umefanikiwa.
"..Mtandao unatambua kuwa kuna mapungufu yaliopo lakini kubwa zaidi ni
kwamba ukilinganisha naKatiba ya Mwaka 1977, Katiba Pendekezwa
imemtambua Mwanamke na imempa nafasi stahiki kushiriki katika kujenga,
kulinda, kuilinda na kuitetea demokrasia inayozingatia haki za usawa,"
alisema
Dk. Maria Semakafu.
Akitolea mfano alisema madai ya msingi 12 ambayo mtandao ulipaza sauti
kutaka kuingizwa ni pamoja na haki za Wanawake kuainishwa kwenye Katiba
Mpya, sheria Kandamizi kubatilishwa, kulindwa kwa utu wa mwanamke,
utekelezwaji wa mikataba ya kimataifa kuhusu haki za wanawake na haki
sawa katika nafasi za uongozi.
Aliongeza kuwa mambo mengine ni haki za watoto wa kike, haki za kufikia, kutumia, kunufaika na kumiliki rasilimali, haki za uzazi salama, haki za wanawake wenye ulemavu, haki za kufikia na kufaidi huduma za msingi, kuwepo kwa tume ya usawa wa kijinsia na kuwa na mahakama ya familia katika katiba mpya.
Aliongeza kuwa mambo mengine ni haki za watoto wa kike, haki za kufikia, kutumia, kunufaika na kumiliki rasilimali, haki za uzazi salama, haki za wanawake wenye ulemavu, haki za kufikia na kufaidi huduma za msingi, kuwepo kwa tume ya usawa wa kijinsia na kuwa na mahakama ya familia katika katiba mpya.
"...Kwa
kiasi kikubwa katiba iliyopendekezwa imezingatia masuala mengi
yaliodaiwa na mtandao. Tunatambua juhudi kubwa zilizofanywa na wanawake
na wanaume wote wa Bunge Maalum la Katiba, na kuwapongeza kwa yale yote
waliyoyatetea kwa nguvu zote na hatimaye kuzingatiwa katika Katiba,"
alisema Dk. Maria Semakafu.
Akizungumza
awali kabla ya kumkaribisha Dk. Maria Semakafu, Mkurugenzi Mtendaji wa
TAMWA Valerie Msoka alivipongeza vyombo vya habari kwa kukubali kupaza
sauti juu ya madai anuai ambayo yalitolewa na wanawake ili kuingizwa
kwenye mchakato. "...Tunatambua pia mchango wa vyombo vya habari katika
kujenga ufahamu kuhusu mchakato wa katiba na hasa kuhusu kwanini katiba
mpya izingatie usawa wa kijinsia." alisema Msoka.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment